Ufaulu wa wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2016 Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa umeongezeka ukilinganisha na mwaka jana, ambapo ufaulu kwa mwaka huu ni asilimia 87.43, wakati mwaka jana ulikuwa ni asilimia 85, sawa na ongezeko la asimilia 2.43.
Hayo yalisemwa na Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Mkoa (shule za msingi) Salimin Mndeme, jana wakati akiongea na SIMBAYABLOG kuhusu matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016.
Alisema kuwa kuongezeka kwa ufaulu mwaka huu Manispaa ya Iringa ni kutokana na utekelezaji mzuri wa mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) ulioanzishwa na serikali hivi karibuni, nakuongeza kuwa manispaa ya Iringa imeshika nafasi ya pili kimkoa (ya kwanza kimkoa ni Mafinga Mji).
Alisema kuwa wanafunzi waliofaulu mwaka 2016 ni 2,998 (1,414 wavulana na 1,584 wasichana) ambapo wanafunzi wote waliofaulu mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2017.
Alisema kuwa Manispaa ya Iringa ina jumla ya shule za msingi 50, lakini ni shule 48 kati ya hizo shule za serikali ni 42 na zisizo za serikali ni sita (6) ndio ambazo zilikuwa na wananfunzi waliofanya mtihani ya kumaliza elimu ya msingi.
Alisema kuwa wanafunzi watakaojiunga na elimu ya sekondari ni wale waliofaulu katika madaraja A, B na C ambaye jumla yake ni 2,998 wote watajiunga na elimu ya sekondari mwakani.
Aliongoza kuwa ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka, kwa mfano, mwaka 2014 ufaulu ulikuwa ni asilimia 82.49, 2015 ufaulu ulikuwa asilimia 85 na mwaka huu ufauli ni asilimia 87.43.
Aidha, kaimu afisa elimu alisema kuwa jumla ya wanafunzi 3,440 (wavulana 1,624 na wasichana ni 1,816) waliosajiliwa kufanya mtihani lakini waliofanya mtihani huo ni 3,429 (wavulana 1,618 na wasichana 1,811) sawa na asilimia 99.7.
Katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi walitahiniwa katika masomo matano ambayo ni Kiswahili, maarifa ya jamii, kiingereza, hisabati na sayansi.
Aliongeza kuwa wanafunzi wengi walifanya vibaya katika masomo ya Kiingereza na Hisabati wakati masomo waliyofanya vizuri ni Kiswahili, Maarifa ya Jamii na Sayansi.
Hata hivyo, kaimu afisa elimu alisema kuwa Manispaa ya Iringa inaupungufu wa walimu wataalamu katika masomo ya Kingereza na Hisabati pengine ndio sababu za wanafunzi wengi kufanya vibaya katika masomo hayo.
Alishauri kuwa ili kuongeza ufanisi katika utendaji kwa walimu serikali hainabudi kuwafanyia semina mara kwa mara yaani (in-service training) kwa walimu katika masomo ya kingereza na hisabati ili kuongeza ufanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment