Lucia Mlowe, mbunge viti maalumu (Chadema) mkoani Njombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Matiganjola katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe jana. (Picha na Friday Simbaya)
|
NJOMBE: WANANCHI wa Kijiji cha Matiganjola katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe wameiomba serikali kuwapelekea umeme ambao utasaidia kuwapo kwa huduma mbalimbali kijijini hapo ikiwepo kupandisha maji ya kisima.
Wananchi hao wamesema kuwa kuto kuwapo kwa umeme kijijini hapo hata huduma ya maji inakosekanana pamoja na kuwapo kwa Tanki Kubwa ambalo lilijengwa miaka zaidi ya 15 iliyopita na hakuna maji.
Wananchi wanatoa ombi lao kwa serikali mbele ya mbunge wa Viti maalum mkoa wa Njombe, Lucia Mlowe ili kufikisha suala hilo serikalini kupitia Bungeni.
Lazaro Mwinami, Samson Nyagawa na Agustino Mgaya, ni baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Matiganjola waliosema kuwa nyumba zao zimepewa namba kwa muda mrefu kupitia shirika la umeme nchini (TANESCO), lakini hawajapata umeme huo.
Lucia Mlowe, mbunge viti maalumu (Chadema) mkoani Njombe alisema kuwa masuala hayo ameyapokea na atafikisha kila jambo panapo husika ili kuzitatua kero hizo.
No comments:
Post a Comment