Friday, 2 December 2016

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUTATUA MGOGORO KIWANDA CHA KARATASI






Afisa Mipango Miji na Vijiji wa Wilaya ya Kilolo, Bernard Kajembe akiendesha mdahalo katika Kijiji cha Makungu kata ya Makungu tarafa ya Kasanga wilayani Mufindi, mkoani Iringa.Mdahalo huo wa nini kifanyike ili kupunguza migogoro ya ardhi ulionadaliwa na shirila lisilo la kiserikali la TAGRODE la mkoani Iringa hivi karibuni. (Picha na Friday Simbaya)


Mwananchi wa Kijiji cha Makungu kata ya Makungu tarafa ya Kasanga wilayani Mufindi, mkoani Iringa akitoa maoni yake wakati wa mdahalo wa nini kifanyike ili kupunguza migogoro ya ardhi ulionadaliwa na shirila lisilo la kiserikali la TAGRODE la mkoani Iringa hivi karibuni. (Picha na Friday Simbaya)




MUFINDI: Wananchi wa kijiji cha Makungu kata ya Makungu tarafa ya Kasanga wilayani Mufindi, mkoani Iringa wameomba serikali kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya kijiji hicho na Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi paper mills LTD (MPM).

Wananchi hao walisema hayo wakati wa mdahalo wenye lengo la nini kifanyike ili kupunguza migogoro ya ardhi ya kijiji ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la TAGRODE la mkoani Iringa kwa kushirikiana shirika na PELUM la Morogoro hivi karibuni.

Mdahalo huo ni wa kumi (10) na wa mwisho tangu kuanza kwa midahalo hiyo inayoandaliwa na shirika la TAGRODE lenye makao yake mkoani Iringa inayolenga kutafuta mambo yakufanya ili kupunguza migogoro ya ardhi katika wilaya za Iringa na Mufindi mkoani Iringa.

Shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la PELUM Tanzania la mkoani Morogoro kwa ufadhali wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), limeendesha midahalo hiyo katika vijiji vya Ikuka, Mbigili, Mawala, Mawambala na Masalali kwa Wilaya ya kilolo.

Huku vijiji vya Usokami, Ugesa, Makungu, Magunguli na Isaula katika Wilaya ya Mufindi kupitia mradi wake wa CEGO unaohusisha jamii ya vijijini katika uwajibikaji wa masuala ya ardhi ya kijiji.

Walisema kuwa mgogoro huo umedumu miaka nane sasa bila kutatuliwa kunakopelekea kuwepo kwa mahusiano mabaya kati ya wananchi wa kijiji cha Makungu na mwekezaji.

Wananchi hao walidai kuwa serikali ya kijiji hicho ilitoa ardhi kubwa kwa wawekezaji bila wananchi kushirikishwa kikamilifu na kusababisha baadhi wananchi ambao walikuwa wanaishi maeneo hayo kukosa maeneo ya kulima pamoja malisho ya mifugo yao.

Aidhi, viongozi wa kijiji cha Makungu akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Donatus Mnoga na Mtendaji wa kijiji (VEO) Mwagala Hemed walithibitisha kuwepo kwa mgogoro huo wa ardhi kati ya kijiji na kiwanda cha karatasi ulioanza tangu mwaka 2008.

Viongozi hao wa kijiji wameiomba serikali ifike kijijini hapo ili kuweza kumaliza mgogoro uliopo kati ya wananchi wa Makungu na kiwanda cha karatasi cha Mgololo ili kuweza kuleta mahusiano mazuri baina ya pande mbili hizo.

Viongozi hao wamekiri kuwa wapo baadhi ya wananchi walilipwa fidia baada ya kuhamishwa katika maeneo yao na wengine bado wadai fidia hizo bila mafanikio na kusahauri kwamba serikali ya Wilaya ya Halmashauri ya Mufindi na ile ya mkoa wa Iringa ziweze kumaliza mgogoro huo kabla haujafikia hatua mbaya.

Hivi karibuni kumetoa moto katika Kijiji cha Makungu uliounguza shamba la miti la mwekezaji liliopo katika kijijini hapo uliosababisha wananchi kumi kujeruhiwa wakati wakijaribu kwenda kuzima moto huo.

Kwa mujibu wa serikali ya Kijiji cha Makungu, ilisema kuwa kijiji hicho kilipeleka wananchi wake 60 kwenda kusaidia kuzima moto uliokuwa ukiunguza miti katika shamba la kiwanda cha karatasi cha Mgololo (MPM), ndio walipopata ajali ya gari baada ya lori waliokuwa wakisafaria kupinduka na kusababisha majeruhi wakiwemo wafanyakazi wawili kiwanda hicho.

Wananchi hao kwa kushirikiana na wafanyakzi wa kiwanda hicho waliffanyikwa kuzima moto huo ngawa watu wanne walijeruhiwa na moto ambao wanaendelea na matibabu kati hospitali ya Mafinga.

Na baadhi ya majeruhi katika ajali ya gari pia wamelazwa katika hospitali ya Wilaya Mufindi wakiendelea na matibabu.

Kwa upande wake, Mkuregenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Yerra Choudary aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Makungu kwa kuonesha ushirikiano wakusaidia kuzima moto katika shamba la miti ya kiwanda hicho ambayo ipo kijiji hapo.

Aidha, mkurugenzi mtendaji huyo pia waliwapa pole wananchi waliopata ajali ya gari wakati wakienda kusadia kuzima moto uliokuwa unateketeza shamba la miti la kiwanda hicho, amabpo hata hivyo chanzo cha moto huo hakijulikani.

Kiwanda cha karatasi cha Mufindi paper Mills LTD (MPM), zamani Southern Paper Mills (SPM) kilichokuwa kinamilikiwa na serikali ya Jamhuri ya Tanzania, chini ya shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kilichopo Wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa kwa sasa kina milikiwa na Kampuni ya RAI GROUP LIMITED.

Kiwanda hiki cha Mgololo kilianzishwa rasmi na kuzinduliwa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius. K. Nyerere mwaka 1985, kikiwa na jukumu la kuzalisha karatasi kwa kutumia malighafi za ndani na nje ya nchi kwa uchache, lengo ilikuwa ni kufanya biashara na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Hivi karibuni Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini limekitoza faini ya shilingi milioni 20 Kiwanda cha Karatasi Mufindi (MPM) kilichopo kijiji cha Mgololo kata ya Makungu katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa baada ya kushindwa kufanya maboresho katika mfumo wake wa kuchuja majitaka kabla ya kuingia kwenye mto Kigogo licha ya kuagizwa kufanya hivyo mara kadhaa.

Kwa mujibu wa NEMC, ilisema kuwa kiwanda hicho pekee cha uzalishaji wa karatasi nchini kimeshindwa kudhibiti majitaka yanatoka kiwandani hapo na kutiririshwa katika mto Kigogo, hali ambayo imesema inayaweka rehani maisha ya watu na viumbe wengine wanaotumia maji ya mto huo.







No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...