Sunday, 29 January 2017

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO



Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani Iringa Kennedy Komba akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum kuhusu mikakati iliyowekwa na jeshi hilo kupambana na majanga ya moto mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya) 




Na Friday Simbaya, Iringa 

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Iringa Mrakibu kennedy Komba ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa askari wanaokuwepo kwenye eneo la tukio. 

Alisema kuwa wananchi wanaokuwepo eneo la tukio huchelewa kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutokana na kuanza kwanza kuokoa mali zilizomo ndani ya Jengo linaloungua bila kutoa taarifa kwanza kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. 

Mrakibu huyo alitoa kauli hiyo wakati wa mahojiano maalum na nipashe ofisini kwake jana na kuongeza kuwa wananchi wanabudi kutoa ushrikiano kwanza ili askari waweze kuokoa mali, hasa katika majanga ya moto. 

Alisema kuwa ujenzi holela na uwekwaji wa vikwazo kama vile matairi chakavu, kanopi, vyuma na mawe makubwa kando ya mitaa finyu ya maeneo hayo ni sababu mojawapo zinazochelewesha zoezi la kuoaji. 

Katika hatua nyingine, Mrakibu Kennedy Komba amewata wananchi na makapuni kuleta mchoro yao ya nyumba kwa jeshi hilo ili wawezo kuelekezwa sehemu ya kuweka vifaa vya moto. 

Kamanda huyo amewataka wamiliki wa majengo na nyumba mkoani Iringa kuhakikisha wanafunga vifaa vya zima moto ili kujiadhari na majanga ya moto mara yanapotokea. 

Komba alisema katika kuuweka mkoa wa Iringa salama na janga la moto, jeshi la zimamoto linaendelea kutoa elimu na mafunzo kwa umma ili kuaondoa tatizo la janga la moto. 

Alisema lengo la mafunzo na elimu hiyo ni kuwapa uelewa jinsi ya kuepukana na majanga ya moto katika jamii. 



Kamanda alisema vifaa vinavyotakiwa kuweka katika majengo na nyumba kwa ajili ya kujikinga na majanga ya moto ni pamoja na ndoo ya mchanga mkavu, Fire Extingusher pamoja na viashiria vinavyotoa sauti kama king’ola. 

Aidha Komba amesihi wamiliki wa vyombo vya usafiri na usafirishaji kuhakikisha wanapeleka vyombo vyao kufanyiwa ukaguzi na kupewa fomu maalum ya ukaguzi, na kununua vifaa vya kudhibiti janga hilo ili kuondokana na athari. 

Hata hivyo, kamanda huyo jeshi la zimamoto na uokoaji amewataka wananchi kutotumia namba ya dharura 114 kutoa taarifa za uongo kwa jeshi hilo badala yake watumie vizuri kwa kutoa taarifa zitakazofanya jeshi kufika haraka kwenye matukio hayo.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...