Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi kulia akisikiliza kilio cha wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya alipotembelea kujionea na kusikiliza changamoto za huduma za afya katika jimbo lake ili kuzitafutia ufumbuvi na kuboresha huduma hiyo.
Na fredy mgunda,Iringa
MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi alifanya ziara ya kuzitembelea zahati,vituo vya afya na hospitali za jimbo hilo kwa lengo la kujionea changamoto za kiafya.
Akiwa katika ziara hiyo alikumbana na changamoto ya kukosekana kwa umeme katika baadhi zahati za jimbo hilo na kuahidi kulipeleka tatizo hilo bungeni ili litafutiwe ufumbuzi mapema.
Akizungumza na blog hii Chumi alisema tatizo la umeme katika vituo na zahati ni kubwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada kutatua tatizo la umeme ili kuboresha afya za wananchi wake pamoja na huduma ya mama na mtoto.
“Hii inasikitisha sana hebu angalia zahati zinavifaa vyote mhimu ila umeme ndio tatizo hatuwezi kupata huduma bora kama hakutakuwa na umeme tunaelekea bungeni nitaenda kuongea na waziri husika ili kutatua changamoto hii” alisema Chumi
Aidha mh chumi alisema kuwa anapenda kuhakikisha kuwa umeme wa REA awamu ya tatu unazifikia zahati zote pamoja na vijiji husika kwa kuwa serikali inalengo la kusambaza umeme vijiji vyote nchi nzima hivyo hata vijiji vya jimbo la Mafinga Mjini vimo katika mpango huo.
Nao baadhi ya Wananchi walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ndani ya mwaka mmoja tu amefanya vitu vingi vizuri tofauti na matarajio ya watu wengi.
“Angalie nyie waandishi wa habari Mbunge Cosato Chumi kwa mwaka moja tu ametengeneza barabara karibi a zote za jimbo huku nyingine zikiwekwa rami,amehangaikia swala la maji tunaona matumaini,swala afya ndio kafanya vitu vingi,michezo ndio mechi zinaendelea na mambo mengine mengi huyu mbunge ni wakuigwa kwa juhudi zake” walisema wananchi
Wananchi hao waliongeza kuwa swala la umeme mbunge wetu ametueleza vizuri sana hivyo tunaimani ya maneno na vitendo yake kuwa analishughurikia kwa umuhimu mkubwa.
Baadhi ya madiwani wa jimbo hilo walisema kuwa kuwa mbunge huyo amekuwa akiwasaidia kutatua changamoto nyingi za kitendaji na kuifanya kazi yetu ya udiwani kuwa rahisi kutokana na mambomengi anayafanya mbunge wetu Cosatio chumi.
“Tunamshukuru Mbunge wetu kwa kuwasaidia wananchi taa za sola kwa vijiji ambavyo havina umeme hizo ni juhudi zake binafsi na sio hilo kafanya mambo mengi sana hadi sasa tunajiona tupo kwenye halmashauri kongwe kumbe ni halmashauri mpya” walisema baadhi ya wadiwani
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.
No comments:
Post a Comment