Sunday, 12 February 2017

21 MANISPAA YA IRINGA WANASWA KWA KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA




IRINGA: Wakati vita dhidi ya madawa ya kulevya ikiendelea nchini, Jeshi la polisi mkoani iringa limewakamata watuhumiwa 21 wanaouza na kutumia madawa ya kulevya katika operesheni maalum yakutokomeza biashara ya madawa ya kulevya. 


Akizungumza na SIMBAYABLOG leo kamanda wa polisi mkoa wa iringa, ACP Julius Mjengi alisema kuwa katika opersheni hiyo iliyoendeshwa kati ya tarehe 6 na 7 februari mwaka huu katika manispaa ya iringa ambapo jeshi hilo liliwanasa watuhumiwa 21 wanaojiuhusisha na biashara ya madawa ya kulevya. 


Kamanda huyo alisema kati ya watuhimiwa hao saba (7) wanatuhimiwa kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya aina ya heironi na wengine 14 wanatumia madawa ya kulevya. 


Hata hivyo alisema kwa sasa ni mapema kutaja majina ya watuhumiwa hao wa dawa za kulevya kwani bado wanaendelea na zoezi la kuwahoji ili kupata mtandao mzima wa wauzaji wa dawa hizo kabla ya kuwafikisha mahakamani wote kwa pamoja . 

Alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Iringa likiwemo eneo la Miyomboni , Mwembetogwa , Mlandege , Mshindo , Ipogolo ,kitanzini na Kihesa na kuwa zoezi la kuwakamata wote waliotajwa kwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ama uuzaji linaendelea . 

Kuhusu aina ya dawa ambazo walikuwa wakiuza alisema watuhumiwa hao wote hakuna aliyekamatwa na dawa za kulevya na katika mahojiano wote wanadai kuwa walikuwa wakijihusisha na biashara hiyo zamani la kwa sasa wameiacha kabisa . 

Kamanda huyo alisema mbali ya kutokutwa na ushahidi bado hawataachiwa huru watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao . 

Aidha aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara pamoja na matumizi ya dawa za kulevya kwani alisema oparesheni hiyo inayoendelea ni mkoa mzima wa Iringa 

Wakati huohuo, jeshi la polisi mkoani iringa linamsaka mtu anayedaiwa kuleta dawa za kulevya kutoka jijijni Dar es Salaam hadi iringa ili mkono wa sheria uweze kuchukua mkondo wake juu ya mtuhumiwa huyo.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...