Saturday, 4 March 2017

KIJIJI CHA ISIMIKINYI WAPITISHA SHERIA NDOGO ZA MALIASILI

Afisa Habari wa Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT), Edina Tibaijuka akiongea na wananchi wa kijiji cha Isimikinyi wilayani Mufindi, mkoani Iringa wakati mkutano mkuu wa kijiji hicho jana. (Picha na Friday Simbaya)

Mmoja ya misitu ya Kijiji cha Isimikinyi wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyohifadhiwa na wananchi wa kijiji hicho. (Picha na Friday Simbaya)



Mtendaji wa Kijiji cha Isimikinyi, Gustav Fabian Mdemu akisoma mapendekezo ya sheria ndogo yaliyopendekezwa na halmashauri ya kijiji hicho na hatimaye kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji jana. (Picha na Friday Simbaya)



Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Isimikinyi wakimsikiliza Mtendaji wa Kijiji cha Isimikinyi, Gustav Fabian Mdemu wakati akisoma mapendekezo ya sheria ndogo yaliyopendekezwa na halmashauri ya kijiji hicho na hatimaye kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji jana. (Picha na Friday Simbaya)





MUFINDI: Wananchiwakijiji cha Isimikinyi, Kata ya Malangali wilayani Mufindi, mkoani Iringa wamepitisha sheria ndogo ya usimamizi wa maliasili (misitu na wanyamapori) ilikukabiliana na kasi ya uharibifu wa rasilimali hizo.

Sheria ndogo hizo za halmashauri ya kijiji cha Isimikinyi zi melenga kuhifadhi na kuendeleza misitu ya Chanunu, Mlimba na Nzali inayohifadhiwa na kijiji hicho.

Hatua hiyo ilifikiwa tarehe jana katika mkutano mkuu wa kijiji ambapo Mtendaji wa Kijiji hicho, Gustav Fabian Mdemu kwa kushirikiana na mwenyekiti wa kijiji hicho Fred Msewa waliwasomea rasimu ya mapendekezo ya hizo za ndogo kwa wananchi kabla ya kuzipitisha.

Misitu ya kijiji cha Isimikinyi ya Chanunu, Mlimba na Nzali ina jumla yahekta 208, ambapo sheria hizo zilizopitishwa na wananchi itakayotumika katika usimamizi wa maliasili ya misitu hiyo iliyohifadhiwa vizuri na kijiji hicho.

Mchakato wa uboreshaji sheria ndogo hizo ulifanywa naTimu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Mwanasheria wa Wilaya ya Mufindi, Shirika la Mufindi Vijana kwa Maendeleo (MUVIMA) pamoja na wananchi.

Kupitia mkutano mkuu wa kijiji, wananchi pamoja na LEAT na mwanasheria wa wilaya waliangalia upya sheria zilizokuwazikitumika kijijini hapo na kugundua kuwa zilikuwa na mapungufu. 

Sheria hizo zinaelekeza haki na wajibu wa wananchi, serikali ya kijiji, kamati ya maliasili pamoja na timu ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii. 

Pia sheria zimefafanua adhabu zitakazotolewa kwa watu watakaokiuka sheria na kuharibu maliasili ya misitu. 

TimuyaWanasheriaWateteziwa Mazingira kwaVitendo (LEAT) inatekeleza mradi wa Ushirikiwa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili (CEGO-NRM) katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi mkoani Iringa.

Mradi huu umefadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID). 

Lengo la mradi ni kuzijengea uwezo jamii zinazoishi karibu na rasilimali misitu na wanyamapori, iliwaweze kuzisimamia na kunufaika nazo. 

Mradi huu kwa kushirikiana na asasi zilizoteuliwa LEAT unatoa mafunzo ya sheria, sera, miongozo, kanuni na Ufuatiliaji uwajibikaji jamii kwa kamati za vijiji za maliasili na mazingira, uchumi, majina matumizi ya ardhi. 

Aidha, Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na shirika la Mufindi Vijana kwaMaendeleo (MUVIMA) walitoa mafunzo ya sheria, sera, miongozo, kanuni na Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii.

Walisema kuwa kupitia mafunzo hayo wameweza kuwawawezesha wananchi kutambua haki zao mbalimbali ikiwemo ummliki wa ardhi.

Kuhusu sheria ndogo walizozipitisha, wananchi hao walisema kuwazitasaidia kupunguza uharibufu wa mazingira pamoja na kulinda vyanzo vya maji.

LEAT imewezesha halmashauri za vijiji vya Lugodalutali, Igombavanu, Tambalang’ombe, Mapogoro, Uhambila na Isimikinyi kupitisha sheria ndogo.

Aidha vijiji ambavyo havijapitisha na vipo kwenye mchakato wa kupitisha sheria ndogo kupitia mikutano mikuu yao ni pamoja na Itengule, Idumlavanu, Ihefu, Mwitikilwa na Tambalang’ombe vilivyopo wilayani Mufindi, mkoani Iringa.



Mwisho

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...