Na Friday Simbaya, Iringa, zana haramu za uvuvi za chomwa moto Migoli
IRINGA: Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amepiga marufuku uvuaji wa samaki wachanga walio chini ya kiwango kinachoruhusiwa cha inchi tatu (3) kuankochangia uharibifu wa mazalia ya samaki katika Bwawa la Mtera.
Alisema kuwa kwa muda mrefu Bwawa la Mtera limekuwa likikabiliwa na tatizo la uvuvi haramu unaotumia zana haramu za uvuvi kama vile nyavu za kokoro, gonga, kimia na katuli.
Kasesela alitoa agizo hilo jana wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi 124 kwa moto lililofanyika katika Kijiji cha Migoli, Taarafa ya Isimani wilayani Iringa, mkoani Iringa.
Alisema kuwa uvuvi haramu umepelekea kupunguza kiwango cha samaki katika Bwawa la Mtera kwa kuvua samaki wachanga walio chini ya inchi tatu (3) na kupelekea uharibifu wa mazalia ya samaki.
“Uwepo wa bwawa hili umekuwa na faida kwa jamii, umewezesha shughuli za uvuvi kuwaongezea kipato na kuboresha lishe katika jamii kwa vile karibu asilimia 90 ya wananchi wa vijiji vinavyoishi karibu na bwawa hilo vinalitegemea,’ alisema Kasesela.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina eneo la kilometa 220 za bwawa hilo ambapo linajumuisha Kata ya Migoli katika vijiji vya Kinyali, Mbweleli, Makatapola, Mtera, Mtera, Migoli na Mapera na Kata ya Izazi katika vijiji vya Mnadani na Makuka.
Naye, Diwani wa Kata ya Migoli, Majaliwa Lyaki (CHADEMA) alisema kuwa zoezi la kupiga marufuku uvuvi haramu katika Bwawa la Mtera halitakuwa na tija kama upande wa pili la bwawa hilo wanaendelea kuvua samaki kwa kutumia zana haramu za uvuvi.
Alisema kuwa Bwawa la Mtera lipo katika eneo linalozinguka Halmashauri za Chamwino na Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma na Halmashauri ya Iringa katika mkoa wa Iringa.
“Ili kuwepo na uvuvi endelevu katika Bwawa la Mtera uvuvi haramu katika upande wa halmashauri za chimwino na Mpwapwa Mkoa wa Dodoma lazima udhhibitiwe…, ” alisema Lyaki.
Kwa upande wake, Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mathew Sanga alisema kuwa katika kudhibiti uvuvi haramu wamefanyikwa kukamata zana haramu 124 na samaki wachanga kilo 7,227 na watuhumiwa 16 walikamatwa.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walipelekwa mahakamani ambapo kati yao 12 walikutwa na makosa na nne (4) kesi zao bado zinaendelea mahakamani.
Sanga alibaini kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inakabiliwa na uvuvi haramu na hili kukomesha vitendo hivyo wamekuwa wakifanya doria na kutoa elimu kwa wavuvi, wafanyabiashara na wasafirishaji wa samaki.
Aidha Halmashauri iliitisha mkutano tarehe 29.03.2017 ambapo wavuvi na wasafirishaji 121 walishiriki, lengo likiwa ni kutoa elimu kwa wasafirishaji wa samaki, wanunuzi wa samaki na wavuvi kuzingatia sheria namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009.
Kanuni hizo zinamtaka kila mmoja kufanya biashara akiwa na leseni ya uvuvi na biashara ya samaki pamoja na matumizi ya nyavu zenye inchi tatu ili kutovua samaki wachanga.
Bwawa la Mtera lina ukubwa wa kilometa za mraba 660 na linalozunguka Halmashauri za Chamwino na Mpwapwa katika Mkoa wa Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika Mkoa wa Iringa.
|
No comments:
Post a Comment