Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdullah Quran pamoja na vitabu mbalimbali vya dini katika mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Dhi Nureyn Foundation uliojumuisha matawi yote ya Tanzania nzima uliofanyika makao makuu Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)
IRINGA: Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya mjini Iringa Shams Elmi amewataka viongozi wa madhehebu ya dini kuhakikisha wanadumisha utulivu uliopo nchini kwa kuhubiri amani na upendo kwa watu wote.
Alisema viongozi wa dini wana mchango mkubwa katika jamii, hivyo wanapaswa kuilinda na kuidumisha amani iliyopo na kwamba jukumu walilonalo viongozi ni kuhakikisha jamii wanayoizunguka inaishi katika mazingira ya utulivu na amani kama ndugu.
Elmi alitoa rai hiyo jana katika mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Dhi Nureyn Foundation... ikijumuisha matawi yote ya Tanzania nzima uliofanyika makao makuu Iringa...ambao ulichukua siku mbili kuanzia tarehe 1-2/4/2017.
Alisema mkutano mkuu huo ulikuwa na malengo ya kuthamini mafaniko na changamoto za Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation.
Mkutano huo walifunguliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyn Islmaic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri na kuhudhuria na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza kwa upande wa serikali.
Taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya mjini Iringa ilianza tangu mwaka 1984.
No comments:
Post a Comment