Friday, 2 June 2017

TRA MKOANI IRINGA YAVUKA LENGO KWA KUSANYA BILIONI 4.7 MWEZI MEI



IRINGA: MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Iringa imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi billion 4.7 katika mwezi Mei mwaka huu huku ikivuka lengo la kukusanya shilingi bilioni 4.5 katika mwezi huo.

Akizungumza na Nipashe kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato jana, Kaimu Meneja wa mkoa wa Iringa Lamson Tulyanje alisema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo iliyopangiwa na serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017.

“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha, kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na wanaokiuka kutumia mashine za kodi za keielektroniki, kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu pamoja na kuhakikisha inaboresha zaidi mifumo itakayompa urahisi mlipakodi katika zoezi zima la ulipaji kodi wa hiari, alisema kaimu meneja Tulyanje.

Tulyanje aliendelea kusisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutoa na kudai risiti za EFD pindi wanaponunua au kuuza bidhaa pamoja na huduma ili kuongeza mapato ya nchi.

Hata hivyo, kaimu meneja huyo aliwataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD.

Kwa upande wa wananchi, kaimu meneja wa TRA mkoa wa Iringa amewaasa kuadai risiti kila wanunuwapo bidhaa au kupata huduma na kuhakikisha usahihi wa kiwango walicholipia sambamba na risiti walizopewa.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...