Monday, 24 July 2017

HATIMAYE LIPULI FC WAPATA VIONGOZI WAPYA


Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU mkoa wa Iringa wakiwa wameweka ulinzi mkali ukumbi wa Shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa unaotumika kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu ya Lipuli FC jana. (Picha na Friday Simbaya)

Mmoja ya viongozi wa Lipuli FC waliomaliza muda wao akitimiza haki yake yakuchagua viongozi wapya jana katika mkutano mkuu ya uchaguziwa klabu hiyo. (Picha na Friday Simbaya)


Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa timu ya mpira ya Lipuli wakifuatilia hotuba ya mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah jana. (Picha na Friday Simbaya



HATIMAYE Klabu ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa jana wamemchagua Ramadhan Mahano kuwa mwenyekiti mpya wa klabu hiyo baada ya kuwagalagaza wapinzani wake wawili. 

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa na kushuhudiwa na mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ambae aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah.

Jumla ya wajumbe na wananchama 171 walishiriki mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu hiyo kongwe nchini na kuapata viongozi wapya watakayedumu kwa miaka mine ijayao. 

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi huo Wakili Jackson Abraham Chakula alisema kuwa Mahano ameshinda kwa kura 103.

Wakati mpinzani wake Nuhu Muyinga akimfuata kwa kura 60 wakati Abnery Mrema akiambulia kura nne (4)tu.

Huku makamu mwenyekiti ambaye aligombea nafasi hiyo pekee yake Ayubu Kihwele akishinda kwa kura 116 huku kura zaidi ya 50 zikiharibika. 

Wajumbe wote wanne waliyogombea wamepita katika nafasi ya ujumbe wa kamati tendaji ambao ni Renatus Kalinga, Sylvester kanyika, Shaban Lushino na Magid Matolla. 

Awali mgeni rasmi katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abudallah aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi watakao ifanya Lipuli kusonga mbele na sio viongozi wa kuendekeza migogoro na kurudisha nyuma Lipuli. 

Alisema kwa kupitia Lipuli FC mkoa wa Iringa utaweza kupiga hatua ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na maeneo mengine mengi ya utalii mkoani Iringa. 

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa Lipuli FC Abuu Changawa alisema amepisha uchaguzi huo yeye na wenzake ili timu hiyo kusonga mbele na iwapo watashindwa kufanya vema basi atafanya mapinduzi kuwaondoa viongozi hao.

Naye Mwenyekiti Mpya wa Lipuli Ramadhan Mahano aliwapongeza wanachama wa Liupuli kwa kutumia demokresia ya kuchagua viongozi wao.

“Tunaomba tupige kazi ya kuiletea Iringa heshima ya mpira kwa wanairinga wote wana kiu kubwa ya mpira…,” alisema Mahono.

Aidha mwenyekiti mpya huyo aliwataka wapinzani wake wazidi kushirikiana naye katika kuinua soka la Lipuli ili iwatangaze kitaifa na kimataifa.

Mahano waliwaomba wanachama na wadau wa soka ndani na nje ya Iringa kuungana kuisapoti timu na uongozi uliopo madarakani kwa kuwa wamechaguliwa kidemokrasia.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...