Monday, 24 July 2017

KAIMU BALOZI ATEMBELEA PROGRAMU ZINAZOFADHILIWA NA MAREKANI MKOANI IRINGA




IRINGA: Kutoka tarehe 20 hadi 21 Julai, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Patterson alifanya ziara mkoani Iringa kwa lengo la kuinua uelewa kuhusu jitihada za Marekani katika kujenga uwezo Watanzania kujenga jamii zenye afya na elimu bora, kuinua uchumi wa jamii na mikoa, kuimarisha taasisi za kidemokrasia na kuwajengea uwezo wanawake na vijana. 

“Wigo mpana wa shughuli zetu nchini na dhamira yetu ya dhati kwa maendeleo ya Tanzania ni kielelezo cha uhusiano wa kina baina ya nchi zetu mbili,” alisema Kaimu Balozi Patterson katika ziara yake katika Shule ya Msingi ya Luganga katika wilaya ya Kilolo, ambako Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) linafadhili mradi wa “Tusome Pamoja” ambao unasaidia kuboresha elimu ya msingi kwa kupitia zana mpya za kufundishia na kujifunzia, mafunzo kwa walimu na wasimamizi wa shule na kuongeza ushiriki wa wazazi na jamii katika uendeshaji wa shule na utoaji elimu. 

“Kwa zaidi ya nusu karne iliyopita, kitovu cha uhusiano wetu kimekuwa ni ubia na ushirikiano wetu na watu wa Tanzania na tuna fahari kuwa wabia wa Watanzania katika jitihada zao za kujenga Tanzania yenye amani, ustawi, usalama na afya zaidi. Ninaamini kwamba dhamira hii itaendelea na uhusiano baina ya nchi zetu utaimarika zaidi.” 

Toka mwaka 2010, Iringa umekuwa mkoa muhimu kwa miradi inayoendeshwa kwa ubia na Serikali ya Marekani, ukiwa na miradi mingi ya mafunzo na maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani, ikiwa ni pamoja na ile inayofadhiliwa na USAID na Peace Corps. Ushirikiano wa maendeleo na wabia wa Kitanzania ni sehemu ya uwekezaji na ushirikiano kati ya Serikali ya Marekani na watu wa Tanzania.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...