Sunday, 16 July 2017

RC IRINGA AMPONGEZA RITTA KABATI KWA KUHAMASISHA MICHEZO KUPITIA MASHINDANO



Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akisalimiana na wachezaji timu ya MUCOBA toka wilaya ya Mufindi mkoani Iringa akifuana na Mdhamini Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kabla mchezo wa fainali kati ya Ruaha FC na MUCOBA FC jana. (Picha Friday Simbaya)






MASHINDANO ya Ritta Kabati ‘Challenge Cup’ yamepata mshindi na bingwa wa kwanza wa mashindano hayo ambaye ni Timu Ruaha FC ya mjini Iringa, baada ya kuitoa MUCOBA ya Mufindi kwa mikwanji ya penati 4-2, baada ya kipenga cha mwisho ilikuwa 0-0 jana.

Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza ambapo pamoja na mambo mengine ametoa pongezi katika uwanja wa chuo cha ualimu Kreluu wakati wa fainali kati ya Mucoba FC na Ruaha. 

Alisema alisema kuwa alipendezwa na mashindano hayo na kuwa yameendeshwa kwa uratibu mzuri japo timu ya Polisi FC ndio ambayo ilitaka kuvuruga mashindano hayo. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema timu ya Polisi ilionyesha utovu wa nidhamu katika mashindano hayo jumbo ambalo sio nzuri katika tasnia michezo ambayo ina taka kuwa na ‘fair play’. 

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alipongeza jitihada za Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati kwa kuhamasisha michezo kupitia mashindano yake ya Ritta Kabati Challenge cup 2017.

Masenza alitoa zawadi mbalimabli kama ifuatavyo; mshindi wa kwanza ni Ruaha FC alipewa pikipiki, kikombe na mpira mmoja na pesa taslimu 50,000/-, mshindi wapili ni MUCOBA alipewa pesa taslimu laki tano na mpira na mshindi wa tatu ni timu ya Kitanzini FC ya mjini Iring ilizawadiwa pesa taslimu laki mbill na mpira pamoja na zawadi zinginezo zilizotolewa kwa washindi mbalmbali.


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amepongeza jitihada za Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati kwa kuhamasisha michezo kupitia mashindano yake ya ‘Ritta Kabati Challenge Cup 2017.’

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...