Friday, 11 August 2017

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA IRINGA LAPATA NAIBU MEYA MPYA



Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr.William D. Mafwere (kulia) akizungumza wakati BARAZA Maluum la Madiwani la Manispaa ya Iringa mkoani Iringa jana. Kulia kwake ni Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe na Naibu Meya mpya limemchagua Daddy Igogo Diwani wa kata ya Gangilonga. (Picha na Friday Simbaya)


BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa limemchagua Daddy Igogo Diwani wa kata ya Gangilonga kuwa Naibu Meya mpya wa kwa kura 15 kati ya 26.

Igogo aliyekosa mpinzani baada ya diwani wa kata ya Nduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Bashiri Mtove kujitoa katika kinyang’anyiro hicho alishinda kwa kupata kura 15 na kunyimwa kura 11 kati ya kura 26 zilizopigwa.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Iringa tarehe 10.08.2017 siku ya Alhamisi na uliudhuriwa na wajumbe 26 waliopigakura, ambapo mgombea huyo ameshinda kwa kupata kura 15 za ndio huku kura 11 kati ya 26 zikiwa ni hapana.

Kwa ushindi huo, Igogo anavaa viatu vya Diwani wa Kata ya Kwakilosa, Joseph Lyata (Chadema) aliyekuwa Naibu Meya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaundwa na madiwani 28 kati yao Chadema ina madiwani 21 (14 wa kuchaguliwa, watano wa viti maalumu na wabunge wawili-Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa Mjini na Suzan Mgonakulima mbunge wa viti maalumu).

Na CCM ina madiwani saba ( wanne wakuchaguliwa, viti mmoja na wabunge wawili wa viti maalumu Rita Kabati na Zainabu Mwamwindi) 

Aidha, Naibu Meya huyo ameshukuru wajumbe wote walioudhulia katika Uchaguzi huo kwa kumuamini na kumchagua kuwa Naibu Meya. Pia ameomba ushirikiano kwa wajumbe na Viongozi wa juu kwa siku zijazo.

Mbali na hayo Baraza hilo limefanya uteuzi mpya wa Wenyeviti wa kamati tano za kudumu za Manispaa ikiwemo kamati ya Fedha na Uongozi ambayo itaongozwa.

Alex Kimbe,Kamati ya Mipangomiji na Mazingira itaongozwa na Tandessy Sanga,Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu ambayo itaongozwa na Raphael L. Ngullo, Kamati ya kudhibiti Ukimwi itakayoongozwa na Daddy Johanes Igogo na Kamati ya Maadili itaongozwa na Severin J. Mtitu.



Mwisho

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...