Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah amewasimamisha kazi mwenyekiti wa kitongoji cha kitongoji cha Itungi ilikupisha uchunguzi kwa tuhuma zinazomkabiri kutokana na kushindwa kusimamia shughuli za maenedeleo katika kitongoji hicho.
DC huyo wamefikia hutua hiyo juzi katika mkutano ya hadhara ulioitisha na kitongoji hicho baada ya kuwepo na mgogoro wa uongozi kati ya Kata ya Mlafu na mwenyekiti wa kitongoji hicho katika mamlaka ya mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo, mkoani Iringa.
Alisema kuwa mnamo mwaka 2014 Kata ya Mlafu iliweka mipango ya ujenzi wa bweni na ukarabati wa maabara katika shule ya sekondari Mlafu.
Hivyo kila kitongonji kilipangiwa malengo ya kukusanya fedha kulingana na idadi ya nguvu kazi, hivyo kwa miaka mine sasa kitongoji hicho hakijafanya maendeleo yoyote.
Katika zoezi la kukusanyajiwa fedha hizo vitongoji vya Mlafu na isagwa vilikamilisha michango hiyo ila kitongoji cha Itungi hakikuweza kukamilisha michango hiyo.
Aidha, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Itungi Nerdy Kasian Kipemba (Chadema) alikanusha tuhuma hizo na kudai kwamba uongozi uliopita ndio ulikuwa na matatizo hayo ya kutokusanya michango hiyo kikamilifu.
Kitongoji cha Itungu ambacho kipo Kata ya Mlafu katika mamlaka ya mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo, kinaongozwa na Chama cha Chadema.
Kitongoji hicho kwa sasa kinaongozwa na kaimu mwenyekiti Elia Luka Mposewa mpaka hayo utaratibu wa kumpata mwenyekiti mpya utakapoandaliwa.
Awali, Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ilula Edward Mbembe akisoma taarifa mbele ya Mkuuwa Wilayaya Kilolo Asia Abdallah kuwa kutokana na kitongoji cha Itungi kutokamilisha michango hali hiyo wananchni wa vitongoji vya Isagwa na Mlafu nao waliamua kurudi nyuma katika uchanganyaji wa shughuli za maendeleo ya kata.
Alisema kuwa uongozi wa mamlaka ya mji mdogo wa Ilula na tarafa ya Mazombe ulifika katika kitongoji cha Itungi na kufanya vikao vya ndani na baadae mkutano wa hadhara.
Makubaliano yalifikikwa kwa wananchi ni kuwa mwenyekiti wa kitongoji atoe ushirikiano katika kusanya michango ili shughuli za maendeleo zisikwame.
Mbembe alisema kuwa hali hiyo ya kutotoa ushirikiano katika ukusnayaji michango iliendelea ambapo mtendaji wa kata ya mlafu alimshitaka mwenyekiti wa kitongoji cha Itungi mahakamani na mwisho wa kesi hiyo iliamuru kwenda kukusanya michango hiyo.
No comments:
Post a Comment