Sunday, 20 August 2017

MRADI WA CHANGIA UONGEZEKO LA MAPATO KIJIJI CHA ITAGUTWA





Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagutwa wilayani Iringa, mkoani Iringa Isaya Lubava amesema usimamizi wa maliasili katika kijiji chake umeimarika kwa kiasi kikubwa, hali inayochangiwa na ongozeko la uelewa kwa wananchi kuhusu wajibu wao katika usimamizi wa maliasili.

Alisema hayo jana wakati wa mkutano wa marejeo na kuhitimisha mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili unaotekelezwa na Timu Wanansheria watetezi wa mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa ufadhili wa shirika la Maenedeleo la kimataifa la Marekani (USAID) katika Wilaya za Iringa na Mufindi mkoani Iringa.

Lubava alisema kuwa tangu kwa utekeklezaji wa mradi huo kijiji kimeweza kuongeza ukusanyaji mapato kutokana na kuunda kwa mpango wa usimamizi wa hifadhi ya kijiji.

“Tulibuni njia mbalimbali za usimamizi, yaani ulinzi wa hifadhi na mojawapo ni ufugaji nyuki, ” alisema.

Mradi huyo ulianza kutekelezwa Novemba mwaka 2013 na utafika ukomo mwezi Novemba mwaka huu 2017.

Alisema kuwa kijiji chao kimechukuwa hatutua mbalimbali za kukabiliana na uharibufu wa misitu, hivyo wanajivunia mafanikio katika kukabiliana na matumizi yasiyo dumivu ya maliasili.

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa LEAT imekuwa ikitekeleza mradi wa ‘ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili’ (CEGO-NRM).

Meneja Mradi wa LEAT Remmy Lema alisema mradi umetekelezwa katika vijiji 32 huku lengo kubwa likiwa ni kukuza ushiriki wa wananchin katika uhifadhi wa usimamizi wa maliasili ili kupunguza umaskini na kuhakikisha kuwepo kuwepo kwa usimamizi dumivu (endelevu) wa mazingira.

Alisema kuwa kuhitimishwa kwa mradi huo wa ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili ni chachu ya kuimarisha usimamizi wa maliasili katika mkoa wa iringa na nchini kwa ujumla.

Lema alisema kuwa pamoja na mafankio yaliyfikiwa kupitia mradi huo ni vyema ikumbukwe kwamba jitihad hizo zinapaswa kuibuka kila siku.

Naye mwenyekiti wa bodi wa LEAT, Gosebert Kamugisha wakati wa kuhitimisha alisema kuwa LEAT itaendela kutoa wito kwa serikali kuendelea kuzisaidia taasisi waruzuku wa mradi huo ili ziendelea kutekekleza majukumu yake kikamilifu kwa ajiliya kuyaendeleza malengo ya mradi.

Aidha, Kamugisha alisema kuwa LEAT inaendelea kutoa wito wa kusaidia na kuunga mkono timu za ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii (UUJ) za wilaya na za vijiji zilizoundwa kupitia mradi huo ili ziweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Kamugisha alisema LEAT walikasimisha baadhi ya shughuli kwa waruzuku (subgrantees) wake nne yaani; MBOMIPA, MJUMIKK, MUVIMA NA ASH-TECH wakati wakutekeleza mradi huo. Waruzuku hao walifundishwa juu ya usimamizi wa shirika, fedha na mradi.

Mwisho



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...