WAUZA magazeti mkoani Iringa wameiomba jamii kuthamini kazi yao ya kuuza magazeti na kuachana na dhana potofu ya kuwaona kama ni watu wasiofaa katika jamii.
Wauza mgazeti hao waselima hayo wakati wakiongea na Nipashe jana kupitia umoja wa wauuza magazeti Iringa (UWAMAI), nakuongeza kuwa wameamua kuanziasha umoja huo ili kuondoa dhana potofu ya jamii juu yao.
Walisema kuwa wapo watu wanaowafananisha na wahuni, wavuta bangi na wasiokuwa na maadili katika jamii na wengine kuwahisi kuwa na itikadi Fulani wa vyama vya siasa.
Akifafanua kuhusu jambo hilo mweneyekiti wa umoja huo wa UWAMAI, Mashaka Kayoka alisema kuwa kazi ya kuuza magazeti ni kazi kama kazi zingine za kujiingizia kipato.
Kayoka aliwaomba wadau mbalimbali wa magazeti pamoja na serikali kuviunga mkono vikundi kama hivyo kwa kuthamini kazi zao yakusambaza magazeti kwa wateji mbalimbali ili wapate habari.
“Tumekuwa tukinyoshewaa vidole na jamii kwamba wauza magazeti ni wahuni na watu wa vurugu, kumbe wala sisi tunafanyakazi yetu yakutuingizia kipato. Sisi pia tuna familia na tunatunza familia zetu kupitia kazi hii pamoja na kusomesha watoto wet shule…,” alisema Kayoka.
Alisema kuwa lengo la kuunda umoja huo ni kusaidiana katika shida na raha akatoa mfano kuwa , mwanachama akiugua au akiunguliwa, akifiwa au akifa umoja huo unamsaidia kwa kutoa kidogo fedha katika kafanikisha matibabu au mazishi.
Naye Katibu wa UWAMAI, Bernard Makoli alisema kuwa umoja wao umesajiliwa rasmi na mamalaka husika na kupewa namba ya usajili IR/IMC/CBO NO.208 na kuruhusiwa kufanya shughuli zake katika Manispaa ya Iringa, na kwa mkoa wa Iringa kwa ujumla.
Makoli aliwaomba wadau wa magazeti pamoja na makampuni mbalimbali ya magazeti kuwaunga mkono katika shughuli zao za kila siku.
“Tunafanya kazi ya kusambaza habari kupitia kuuza magazeti kwa hiyo wenye magazeti waone umuhimu ya kuwasaidia na kuwezesha kwa hali na mali…,” alisema.
Aliongeza kuwa umoja huo pia ufanyakazi ya kuelimisha jamii ili iondokane na umasikini kwa kuhamasisha jamii kupitia kazi zao za vikundi ili kuleta mabadiliko chanya ya maendeleo.
Kwa upande wake mweka hazina wa umoja huo Salum Hamisi alisema kuwa kikundi chao kinapata mapato kupitia ada na michango mbalimbali za wanachama.
Alisema kuwa wanaomba taasisi za kibenki na wadau mbalimbali kuwaunga mkono jitihada zao kwa kuwawezesha ili waweza kutunisha mfuko ili wawezi kukopeshana na hatimaye kujikwamua katika umasikini wa kipato.
Na Friday Simbaya, Iringa
No comments:
Post a Comment