Monday, 25 September 2017

MAJALIWA MGENI RASMI MAONESHO YA UTALII YA KARIBU KUSINI


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya utalii yajukalikanayo kama Karibu Kusini-Tanzania Southern Circuit yanataraijiwa kufanyika kwenye viwanja vya Kichangani, Iringa mjini, mkoani Iringa, kuanzia tarehe 27.09.2017 hadi 02.10.2017 jana. (Picha na Friday Simbaya)




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya utalii yajukalikanayo kama Karibu Kusini-Tanzania Southern Circuit yanataraijiwa kufanyika kwenye viwanja vya Kichangani, Iringa mjini, mkoani Iringa, yatakayofunguliwa tarehe 29.09.2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatatu) Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema maonesho hayo yataanza tarehe 27 Septemba hadi 02 Oktoba, 2017.

Alisema kuwa mikoa ya nyanda za juu kusini (iringa, njombe, mbeya, songwe na ruvuma) kwa kushirikiana na wizari ya maliasili na utalii, shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) pamoja na wadau mbalimbali wanaandaa maonesho.

Masenza alisema kuwa mwaka 2009, mkoa wa iringa uliteuliwa na wizara ya maliasilina utalii kuwa kitovu cha utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini.

Alisema kuwa kutokana na uteuzi huo, mkoa wa iringa umepata heshima ya kuaandaa maonesho hayo.

“Lengo kuu ni kutangaza fursa na vivutio vya utalii vilivyopo katika mikoa ya nyanda za juu kusini ili wananchi na wageni kutoka ndani na nje wavifahamu na kuvitembelea na hivyo kukuza utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini,” alisema masenza.

Alivitaja vivutio vilivyopo katika nyanda za juu kusini kama vile vya kihistoria, kiutamaduni na kiikolojia ambavyo vinafanya upekee wa mikoa hiyo katka utalii.

Maonesho ya utalii karibu kusini yanakwenda sambamba na maandhimisho ya kitaifa ya siku ya utalii duniani mwaka 2017 ikijumuisha pia maoneshoya bidhaa za wajasiriamali kutoka katika mikoa ya nyanda za juu kusini na mikoa minigine ya Tanzania.

Kwa mwaka huu 2017 maadhimisho ya siku ya utalii yanaongozwa na kauli mbiu isemayo, “ UTALII NI NGUZO YA UCHUMI WA VIWANDA.”

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...