IRINGA: Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) pichani amesema kutendo cha polisi kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya mlandege mjini Iringa jana kimemudhalilisha kama kiongozi wa kuchaguliwa na wananchi.
Mchungaji Msigwa ambaye yupo nje kwa dhamana alisema hayo (jumatatu) katika mkutano na waandishi wa habari ofisin kwake nakuongeza polisi wamevunja sheria ya bunge yaani, sheria ya Parliamentary Immunity Powers and Privileges Act of 1988 kwa kuvuruga mkuatano wake.
Alisema kuwa sheria hiyo inampa mamlaka ya kutimiza wajibu wake kama mbunge wakati akiongea na wananchi.
Mbunge huyo alikamatwa na polisi Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa kwa kudai kwamba ametoa maneno ya uchochezi.
Alisema kuwa Hali ya kukamatwa kamatwa ya Wabunge wa Upinzani Nchini Hususani Chadema ilikuwa imetulia baada macho na masikio ya wengi kuelekezwa kwenye kumtibu Mbunge wa Singida masharki ,Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwezi huu mjini Dodoma.
Hali ya kukamatwa kamatwa ni kama imeanza tena ndivyo naweza kusema baada,Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) kukamatwa na polisi leo Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa.
Mchungaji Msigwa alisema kuwa anakusudia kumfungulia mashitaka Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OCD) kwa alichodai kwamba alitumia madaraka vibaya.
“Nipo mbioni kumpeleka mahakamani OCD kwa kutendo cha kunishua jukwaani na kunikamata wakati natimiza majukumu yangu kibunge pamoja na kuvunja sheria ya sheria ya Parliamentary Immunity Powers and Privileges Act of 1988,” alisema Msigwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Iringa Mjini (Bavicha), Leonce Marto alisema kuwa mbunge huyo alikamatwa saa 11:24 jioni na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) aliyekuwa ameambatana na polisi wengine kisha wakampeleka ofisi za mkoa za jeshi hilo.
“Kutoka Mlandege mpaka ofisini kwa kamanda wa mkoa amebadilishwa kwenye magari matatu. Tunahisi atakuwa anasafirishwa ingawa bado anahojiwa. Yupo ndani, sisi tunaendelea kumsubiri nje,” alisema Marto.
Mwenyekiti alibainisha kwamba mpaka wakati huo (saa 12:30 jioni) jeshi hilo halikubainisha sababu za kumshikilia Msigwa.
“Alikuwa na kibali cha kufanya mkutano katika kata tatu kuanzia leo Jumapili mpaka Jumanne. Alianza kuzungumza saa tisa alasiri ilipofika saa 11:24 jioni,RCO akiwa na polisi wengi wakamshusha jukwaani na kuondoka naye,” alisema Marto bila kufafanua sababu za kukamatwa.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi alithibitisha kukamwata kwa mbunge wa iringa mjini nakuongeza kuwa alikamatwa kwa kutoa lugha ya uchocheza kwa kuchonganisha jeshi la polisi na wananchi.
RPC alisema kuwa Mchungaji Peter Msigwa yupo nje kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa masaa sita.
No comments:
Post a Comment