Friday, 6 October 2017

DKT HELEN KIJO BISIMBA AMTEMBELA TUNDU LISSU



MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt Helen Kijo Bisimba (Pichani) amesafiri mpaka Nairobi nchini Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu. ambapo anapatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Mjini Dodoma.

Mwanaharakati huyu maarufu nchini ,katika safari yake hiyo , aliongozana na watetezi wenzake na haki za Binadamu ambapo mara baada ya kumjulia hali Lissu ambaye ni Rais wa chama cha wanasheria nchini,(TLS) , amesema haya

"Leo Mungu amenipa neema kumuona Mh. Tundu Antipas Mughway Lissu nimeuona kwa macho muujiza kuwa Tundu pamoja na marisasi yale yote ameniona na kuniamkia nakunipa pole. Yaani yeye ndio anatupa sisi moyo kuwa Kufa mtu hufa mara moja tusiogope kusimamia haki, "


Pichani ni Mkurugenzi wa (LHRC)Dk Bisimba akiwa na watetezi wenzange mjini Nairobi Kenya


Ameongeza kusema kuwa "kusema ukweli, kutetea wanaoonewa.Nimepata nguvu mpya.Watanzania Tundu anawasalimu. Nimemuona anabariki.Mke wake mpenzi naye anaendelea na huduma kwa moyo mkuu ndiye niliye naye pichani.Waliotenda tendo lile wamrudie Mungu maana yupo tena yu hai na amewaonyesha ukuu wake. Mungu akamilishe uponyaji kwa Lissu."Amesema Dk Bisimba

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...