WADAU wa sekta ya afya wameomba Sheria ya mfuko wa afya jamii (CHF) ya mwaka 2001 kufanyiwa mapitio ili ionesho fedha ya fidia kwa huduma iliyotolewa kwa makundi yenye msamaha itatoka wapi na taratibu za namna fidia hizo zitakavyotolewa ili ziongeze fedha kwa ajili ya manunuzi ya dawa.
Wadau hao walisema hayo jana katika kikao cha kujadili changamoto katika utoaji wa huduma za afya wilayani Iringa kilichoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la TACOSODE kupitia mradi uwajibikaji jamii katika sekta ya afya (CEGO).
Kikao hicho kilijumuisha waganga wa zahanati na vituo vya afya, madiwani,watendaji wa kata, afisa mipango wa wilaya, afisa maendeleo ya jamii, mganga mkuu wa wilaya na mratibu wa CHF.
Walisema kuwa Serikali itenge na kupeleka pesa za fidia kwa huduma za afya zinazotolewa kwa makundi maalum ambayo hupata huduma za afya kutoka kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati.
Kwa vile makundi hayo yamekuwa yatumia fedha nyingi za wananchama wa CHF.
Makundi yenye msamaha hawachangii huduma za afya na kunafanya wanachama au wanachaniaji wa CHF kubebeshwa mzigo kwa vile vituo havitoi fidia.
Sheria ya CHF ya mwaka 2001 kufungu cha 10(1) inazipa kamati za afya za kata mamlaka ya kutoa misamaha kwa makundi maalumu kama vile wajawazito, wazee, walemavu na watoto chini ya miaka mitano.
Kifungu 10 (2) kinazipa kamati hizo kutoa fidia kwa huduma za afya zilizotolewa kwa makundi hayo, lakini sheria hiyo haielezi mahali ambapo kamati hizo zitoa fedha za kufidia huduma zilizotolewa.
Walisema kuwa huko ni kuacha mzigo huo migogoni mwa wanachangiaji wa CHF na kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia mfuko na hivyo kuendeleza wimbi la uhaba wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba.
Kwa upande wake, Mratibu wa mfuko wa afya jamii (CHF) halmashauri ya wilaya ya Iringa Dora Mlomo alisema kuwa kuna uchangiaji hafifu wa wananchi katika mfuko huo kupelekea kushindwa kutoa huduma za afya.
Mlomo alitoa rai kwa wananchii kujiunga na mfuko huo ilikuweza kuboreshaji wa utoaji huduma za afya kwani kwa mwaka kaya inatakiwa kichangia shilingi elfu kumi (10).
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiunga kwa wengi ili fedha zinapatikana kwa wengi ilikweza kuwahudumia hata makundi yenye msamaha.
Naye, diwani wa kata ya mlowa, Charles Nyagawa alisema kuwa wanasiasa ni chanzo cha kuzoretesha maendeleo katika maeneo mbalimbali nchi.
Alisema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaamasisha wananchi wasichagie maendeleo kwa mfano ujenzi wa zahanti au shule na kufanya miradi kushindwa kutekelezeka.
Nyangawa alisema kuwa suala la maendeleo lisichanganywe na siasa isipokuwa wanasiasa waungane kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema kuwa wanasiasa kutoka chama tawala (CCM) na wale wa upande wa pili waunge mkono juhudi za serikali katika kutekeleza sera za chama hicho.
Mratibu kutoka TACOSODE Abrahamu Kimuli Mkutano ulikuwa na lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala yaliyotolewa na TACOSODE wakati wa CEGO katika utekelezaji wa mradi wa afya katika halmashauri za wilaya za Iringa na Kongwa.
Kwa USAID mkutano ulikuwa uliangalia fidia ya CHF kwa makundi maalum yaani fidia, usimamizi na utawala kwa "Sheria ya CHF ya 2001" na kupendekeza njia mbadala.
Alisema kuwa Wizara ya Afya inatakiwa kupitia upya taratibu za fidia, usimamizi na utawala wa CHF kama ilivyoelezwa kwa sheria CHF mwaka 2001 ili kupunguza mzigo kwa wanachama wa CHF.
Naye mkurugenzi mtendaji wa TACOSODE Theofrida Kapinga serikali itenge bajeti angalau ifike kiwango kinachopendekezwa katika Azimio la Abuja ambacho ni asilimia 15 ya bajeti yote ya serikali.
Alisema kuwa serikali inatakiwa kusimamia mapato ya ndani kwa vile wahisani wako mbioni kupunguza uchangiaji wa fedha katika sekta ya afya ili kuweza kujitengemea.
Kapinga alisema serikali ipeleke fedha zote zilizoidhinishwa na kwa wakati ili kuwezesha miradi na huduma za afya kufanyika kama ilivyopangwa ili kuepusha kutoa huduma chini ya kiwango vilivyokushudiwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment