Friday, 13 October 2017

WAZAZI WA KWAMISHA UTOAJI WA CHAKULA SHULENI


Baadhi ya wazazi wakifuatlia kikao cha wazazi katika Shule ya msingi Muungano manispaa ya IRINGA, mkoani IRINGA leo. (Picha na Friday Simbaya)

IRINGA: SHULE ya msingi Munnugano katika manispaa ya Iringa, mkoani Iringa imesitisha mpango wakutoa uji kwa wanafunzi kwa muda kutokana na wazazi kusuasua kutoa michango.

Hayo yalielezwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi muungano Richards Nchimbi wakati wa kikao cha wazazi kilicholenga kutamubulisha kamati mpya ya mpango jamii wa uhamasishaji na utekelezaji elimu (MJUUE) Ushirikiano wa Wazazi na Waalimu (UWAWA) jana kupitia program ya USAID Tusome Pamoja.

Alisema kuwa kutokana na wazazi kutoona umuhimu wa watoto wao kupata uji mwalimu mkuu kwa kushirikiana na kamati ya shule hiyo wamesitisha mpango wa chakula shuleni hadi hapo baadaye.

Nchimbi alisema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 700 lakini ni watoto kumi (10) tu kwa sasa ndio wanaokunywa uji shuleni na kupelekea kushindwa kulipa gharama ya mpishi ya shilingi 60 kwa mwezi.

“Tulikuwa na utaratibu wa kutoa uji kwa wanafunzi wote ambapo kila mzazi anatakiwa kuchangia shilingi 2000 kwa mwezi lakini wazazi wengine wameshindwa kutoa michango wa uji kwa wanafunzi,” alisema Nchimbi.

Naye mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi muungano saidi lawa alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu mibovu ya vyoo vya wanafunzi na walimu, uchakavu wa vyumba vya madarasa na kutokuwa na viwanja vya michezo.

Alisema kuwa kupitia mpango jamii wa uhamasishaji na utekelezaji elimu (MJUUE) wamepanga kukalabati vyoo vya wanafunzi ambapo gharama za ukarabati zitagharimu zaidi ya shilingi milioni mbili (2m/-) ambapo kila mzazi mwenye mtoto anatakiwa kuchangia shilingi elfu tano. (5000/-).

Lawa alisema kuwa ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujisomea serikali kwa kushirikiana na jamii wanabudi kutoa michango ya mali na hali ili kuboresho ufaulu kwa wanafunzi.

Kwa upande wao Washiriki wa Mahusiano ya Jamii (CEF) mradi wa USAID Tusome Pamoja, Winston Ngowo na Sara Ndoto walisema kuwa mradi wa elimu wa miaka mitano unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID).

Walisema kuwa Mradi huu unalenga kusaidia kuboresha stadi za ufundishaji na kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) katika shule za awali na madarasa ya chini ya shule za msingi (1-4), katika mikoa minne ya Tanzania bara (Iringa, Morogoro, Mtwara na Ruvuma) pamoja na shule zote za serikali Zanzibar. 

Pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu , vitabu kwa wanafunzi, malengo zaidi ya mradi wa USAID Tusome Pamoja ni kuimarisha ushiriki wa wazazi na jamii kwenye elimu kupitia kamati za shule, Ushirikiano wa Wazazi na Waalimu ( UWAWA) na jamii yote kwa ujumla.

Hivi Karibuni,USAID Tusome Pamoja ikishirikiana na serikali katika mikoa huu, iliendesha mafunzo ya mpango jamii wa uhamasishaji na utekelezaji elimu (MJUUE) wenye lengo la kuhamasisha jamii katika kubaini changamoto katika sekta ya elimu zinazo athiri ubora wa elimu na ufaulu; Kubaini rasilimali na utatuzi wa changamoto hizo.

Pia mafunzo haya yalilenga (kusaidia jamii ishiriki katika kuandaa mipango ya elimu kwa ajili ya watoto wao hivyo kuimarisha ushiriki wa jamii katika kuboresha utoaji wa elimu.

Kupitia mpango huo USAID Tusome Pamoja unaotekelezwa na shirika la Care International kwa shirikia na RTI International, ilitoa mafunzo ya siku tatu kwa Wawezeshaji Jamii Elimu 968 kutoka shule 481 za msingi za serikali mkoani Iringa.

Walisema kuwa pamoja na mambo mengine wameweza kusaidia kuongoza uandaaji wa dira na mipango kazi ya muda mfupi ya shule zao za msingi.

Na mipango hiyo kuridhiwa na jamii, Wahamasishaji hawa baada ya kupata mafunzo pia wanafanya kazi ya kujitolea ya kuhamasishaji jamii kushiriki katika shughuli zote zinazohusu elimu katika shule zao. Na Friday Simbaya, Iringa

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...