HUKU kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kitwiru zikiingia wiki ya lala salama, Chama cha Mapinduzi (CCM) kinazidi kuongeza nguvu katika kampeni zake kwa kuwapandisha jukwaani makada mbalimbali wanaonadi sera za chama hicho na kumuombea kura mgombea wao, Baraka Kimata.
Baraka Kimata anayepewa nafasi ya kushinda uchaguzi huo kama ilivyo kwa mshindani wake kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bahati Chengula amesema ameamua kuigeuka Chadema na kujiunga na CCM ili apate fursa pana zaidi ya kuwatumikia wananchi wa kata hiyo.
Kimata alikuwa diwani wa kata hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kupitia Chadema kabla ya kujiengua akipinga kile anachodai udikteta wa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Katika uchaguzi mkuu wa 2015, Kimata alishinda udiwani wa kata hiyo kupitia Chadema akipata kura 3,183 dhidi ya kura 2,557 alizopata mgombea wa CCM.
No comments:
Post a Comment