Friday, 10 November 2017

MIMBA ZA UTOTONI KUPUNGUA,SERIKALI YASHIRIKIANA NA MASHIRIKA BINAFSI KUTOA ELIMU,


Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) Koshuma Mtengeti, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam


SERIKALI imejipanga kupunguza mimba za utotoni kwa asilimia 27 kwa kipindi cha miaka mitano kinachoanzia 2017 hadi 2022 lengo likiwa ni kuhakikisha mototo wa kike anapata haki yake ya elimu.


Hayo yamesema leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai wakati wa Kongamano la Mtoto wa Kike , liloandaliwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo Uswidi ( Swedish International Development Cooperative Agency-SIDA).


Mussai amesema kwa sasa serikali imeandaa mpango kazi wa Taifa wa kotokomeza ukatili wa kijinsi kwa upande Mimba za Utoto.


“Katika Mpango huu tumeanza kupunguza mimba kwa asilimia 27 kwa watoto na tunaamini mpango huu utasaidia kundokana na tatizo hili”amesema


Amesema katika kutekeleza mpango huu, Serikali itashirikiana Taasisi zisizo za Kiserikali katika kuhakikisha wanapunguza Mimba za Watoto.


Hata hivyo , Mussai amewataka Watoto wa Kike kujitambua wenyewe kwa kujiepesha na mambo yasio faa ambayo yatapelekea kuongezeka mimba za watoto ambapo amedai zimechangiwa na watoto hao kujiingiza kwenye makundi yasioa faa.


Kw upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwapatia fursa watoto wa kike kukurana na Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Uswid ambapo watapata fursa ya kuelezea mafunzo mbali mbali waliyopata kutokana na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya CDF.


Amesema miradi hiyo ni pamoja na miradi ya kutokomeza, mimba za utotoni, ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia na kuonesha kazi za ujasiriamali walizozifanya ikiwa kama mafanikio ya miradi ya CDF.


“Vile vile katika kongamano hili, wanaume na wavulana wakiwa kama mabalozi wa CDF watapata fursa ya kuelezea ni kwa namna gani wanafanya kazi za kuelimisha jamii pamoja na vijana rika juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia, ukeketaji, mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni ili kufikia dhana ya Taifa ya kuleta usawa wa kiiinsia,” amesema Mtengeti.


Naye Mkurugenzi Mwandamizi kutoka SIDA Carin Jamtin, amesema shirika lao limekuwa likitetea haki za woto kwa kuhakikisha watoto wakike na kiume wanakuwa na haki sawa katika jamii hususani haki ya kupata elimu.


Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo Uswidi ( Swedish International Development Cooperative Agency-SIDA) Carin Jamtin, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, Margaret Mussai, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...