Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) umeadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Kaulimbiu ya Sikuya Malaria Duniani mwaka huu ni Kuwa Tayari Kuishinda Malaria.
Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) unaendelea na mkakati wa kupunguza Malaria kwenye jamii ya Geita. Jitihada hiyo inachangia juhudi za Dunia kufikia malengo ya Mkakati wa Dunia kwa Ugonjwa wa Malaria uliowekwa na Shirika la (WHO) kuwa ifikapo mwaka 2020 Dunia yote ipunguze Malaria na vifo vitokanavyo na Malaria kwa asilimia 40.
Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Geita ilizindua mpango wa Kupambana na Ugonjwa wa Malaria mwaka 2010 wa kunyunyuzia Dawa ya Ukoko kwenye kaya mbalimbali mjini Geita.
Kwa sasa kwenye mwaka wake wa Sita katika Kampeni hiyo kiasi cha US$ 900,000 kimetengwa katika Mpango huo. Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Afya ya Mkoa wa Geita umebaini kushuka kwa takwimu za Ugonjwa wa Malaria kuanzia mwaka 2012.
Hali hiyo imepunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya Watoto na mama wajawazito wanaofikishwa Hospitali kutokanana Ugonjwahuo. Huduma ya Afya imeimarika na vifo vitokanavyona Malaria vimepungua kwa kiwango kikubwa.
“Tunafarijika sana kuwa sehemu ya Mchango ya Mapambano dhidi ya Malaria,” alisema Makamu wa Rais wa Miradi endelevu kutoka Mgodi wa Dhahabu Geita, Bw. Simon Shayo.
“Hatua hii itaendelea kuwa kipeumbele chetu kwa kuwa maendeleo ya uchumi na kijamii msingi wake unajengwa kupitia rasilimali watu yenye Afya.”
Msimu uliopita, GGML ilishirikiana na Taasisi isiyoya Kiserikali ya Abt Associates pamoja na Halamshauri ya Mji wa Geita kunyunyizia kaya 20,000 katika kata za Saba za Mtakuja, Nyamkumbu, Kalangalala, Kasamwa, Bunegezi, Bulela na Bung’wangoko mjini Geita.
Pamoja na unyunyiziaji wa Dawa hiyo, elimu na uhamasishaji kuhusu Ugonjwa wa Malaria vimefanyika kuwezesha jamii kuwa na mwamko na kuunga mkono mradi huo iliuweendelevu.
Zaidi ya Vijana 300 wasichana na Wavulana mjini Geita wamepatiwa mafunzo maalum na kuajiriwa sehemu mbalimbali kutekeleza Mradi huo hatua inayowapatia ujuzi na kipato.
Ugonjwa wa Malaria unabakia kuwa changamoto inayokua kwenye Afya na maendeleo ya jamii kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania hali inayohatarisha uzalishaji na ustawi wa jamii.
Mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano ni kundi linaloathirika zaidi na ugonjwa huo hali inayosababisha vifo vingi.
No comments:
Post a Comment