Mshambuliaji Ramadhani Madebe (23 jezi nyekundu) wa Uchukuzi akiwa katika msitu wa wachezaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joseph Mlimi (2), Mohamed Koshuma (16) na Stephen Mgendi (12) katika mchezo wa michuano ya Mei Mosi uliofanyika kwenye uwanja wa Samora. Uchukuzi walishinda bao 1-0. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Winga Salum Idd wa Tumbaku ya Morogoro (11) akikokota mpira kuelekea langoni mwa Tanesco wakati wa mchezo wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tumbaku walishinda mabao 2-0. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Kikosi cha timu ya soka ya Uchukuzi kikiwa pamoja na kocha wake Mkuu Zenno Mputa (kulia) na Mshauri wa timu Kennedy Mwaisabula (Mzazi), kinachoshiriki katika michuano ya Kombe la Mei Mosi inayofanyika katika viwanja mbalimbali mkoani Iringa. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
IRINGA: Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ameomba wafanyakazi wote na wananchi kwa jumla kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kupokea salamu zake za Mei Mosi katika Uwanja Samora.
Alisema kuwa Mkoa wa Iringa umechaguliwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya kitaifa ya sherehe za siku ya wafanyakazi duniani yaani MEI MOSI mwaka 2018.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaogozwa na kauli mbiu isemayo kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi.
Masenza alisema kuwa kilele cha maadhimisho ya mei mosi mwaka 2018 kitakuwa katika uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Samora, mjini Iringa ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Maadhimisho ya sherehe za mei mosi yatanguliwa na michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, kamba, bonaza la michezo mbalimbali.
Michezo hii ilianza tangu tarehe 17/04/2018, na itaitimishwa tarehe 30/04/2018.
Aidha, mkuu wa mkoa huyo aliongeza kuwa sherehe za mei mosi zitahusisha maonesho ya shughuli, huduma na bidhaa mbalimbali za wafanyakazi, taasisi za umma na binafsi, wawekezaji za wajasiriamali katika Uwanja wa Kichangani uilopo eneo la Kihesa mjini Iringa.
Maandalizi ya sherehe za mei mosi yanaendelea vizuri, kamati mbalimbali zimeundwa kwa maandalizi ya shughuli zote zitakafanyika kabla na wakati wa maadhimisho hayo.
Kwa upande wake, Kaimu Mweneyekiti michezo ya Mei Mosi Kitaifa Joyce Benjamin ameupongeza Mkoa wa Iringa kwa maandalizi mazuri ya sherehe za wafanyakazi duniani.
Alisema kuwa amefurahishwa na maandalizi yaliofanywa na Mkoa wa Iringa na kuongeza kuwa hajawahikuona maandalizi kama hayo tangu aanzekushiriki maadhimisho ya Mei Mosi 2009 kwa ushirikiano mzuri.
Joyce alisema kuwa timu mbalimbali zimewasili kushiriki michezo mbalimbali hayo timu za micchezo zimefika hapa Iringa kushiriki michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, kamba, bonaza la michezo mbalimbali.
Alisema kuwa michezo ni furaha na muhimu kwa wafanyakazi kwa vile inaleta afya na kushirikiano baina ya wafanyakazi na hatimaye kuleta umoja ya kitaifa. Na Friday Simbaya, Iringa
No comments:
Post a Comment