Monday, 7 May 2018

ZIMAMOTO YAWATAKA MAKAMPUNI KUWA NA FIRE PROTECTION MANAGERS WA MOTO



Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye (mwenye kaunda suti) akizungumza na viongozi mbalimbali wa jeshi hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pakazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka, yaliofanyika mkoani Iringa. (Picha na Friday Simbaya)



IRINGA: Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye ametoa wito kwa makampuni na wenye viwanda nchini kuwaajiri wataalamu wa moto (fire protection managers) watakaobaini na kung’amua na kukinga moto katika maeneo yao. 

Alisema kuwa makampuni na viwanda kwa kushirikiana jeshi hilo wanatakiwa kuwaajiri wataalamu wa mambo ya moto kwa lengo la kubaini endapo moto utatokea katika maeneo ya kazi. 

Alisema kuwa wataalamu hao wa mambo ya moto wanatakiwa kupata mafunzo kutoka jeshi hilo ama mahali pengine kwa ajili ya kung’amua na kuzuia moto katika viwanda vyao na makampuni. 

Andenenye alisema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pakazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka, yaliofanyika mkoani Iringa. 

Kamishna huyo hivi karibuni alitembelea banda la zimamoto na kukagua vifaa mbalimbali vya kuzimia moto wakati wa maadhimisho hayo yaliofanyika mkoani hapa. 

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29. 

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu. 

Andengenye alisema kuwa jeshi hilo lilishiriki maonesho hayo ilikuwapa wananchi fursa ya kulijua jeshi lao la zimamoto na uokoaji ambalo lipo chini ya wizara ya mambo ya ndani nchini. 

Aidha, kamishna huyo alitoa kwa wananchi kuhakikisha wanapotaka kujenga nyumba zao za biashara au viwanda kuhakikisha wanapoleka ramani zao ili jeshi la zimamoto na uokaoji ilikague kama ramani hizo zina mifumo ya maji kuzimia moto. 

Hata hivyo, Adengenye alitoa wito kwa mamlaka mbalimbali kwa kushirikiana jeshi hilo kujenga visima vya maji katika maeneo mengi zaidi ili kusaidia jeshi hilo kuzima moto kwa haraka. 

Pia alisema kuwa wenye viwanda na kwenye maghorofa wanatakiwa kupeleka ramani zao kabla hawajaanza ujenzi ili kuaangalia kama rani hizo zina mifumo ya maji kwa ajiri yakuzimia moto. 

Mwisho 



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...