Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe amewaomba wadau mbalimbali kuchangia sekta za elimu, afya na maji pamoja sekta zingine katika manispaa hiyo.
Meya huyo alitoa kauli hiyo jana wakati akifunga mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani la manispaa ya iringa kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Kimbe alisema kuwa wadau wa maendeleo wanaweza kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabilia manispaa hiyo ikiwemo changomto yakutekamilika kwa badhi ya miradi ya maendelea kutokana na uhaba wa fedha.
Alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya iringa imewapongeza wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo kampuni ya ASAS Group kwa kuchangia fedha katika sekta ya afya, maji na elimu.
“Wakati tunalekea katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2017/18 kuna miradi mingi haijakamilika kutokana na uhaba wa fedha na sisi kama halmashauri tunatakiwa kujipanga kuweza kumalizia miradi ambayo haijakamilika,” alisema Kimbe.
Katika hatua nyingine, kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi Halmashauri ya Manispaa Iringa Ibrahimu Ngwada alisema katika kipindi cha robo ya tatu, januari hadi machi 2017/2018 kamati hiyo ilieendelea kutekeleza mikakati ya kupambana na janga la ukimwi kwa kushirikiana na wadau wa mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.
Alisema kuwa huduma za ushauri na upimaji wa hiari zilitolewa, jumla ya watu 4269 wakiwemo wanaume 2145 na wanawake 2124 walipimwa afya zao kwa hiari.
Ngwada aliongeza kuwa waliokutwa na maambukizi ya VVU/UKIMWI ni watu 383 kati yao wanaume 146 na wanawake 237.
Aidha, kaimu mweneyekiti huyo alisema kuwa huduma za tiba sahihi ya magonjwa ya ngono ilitolewa katika vituo vyote vya afya na zahanati, ambapo jumla ya watu 325 wakiwemo wanaume 63 na wanawake 262 walipata tiba sahihiya magonjwa ya ngono.
Wakati huohuo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela ambaye pia ni mshauri katika baraza la madiwani alitoa ushauri kwa baraza hilo kutatua migororo ya viwanja.
Alisema tatizo la viwanja la double allocation ni kubwa kwa kuwa viwanja hivyo vinadaiwa kuwa mkoa unatoa viwanja na manispaa nayo intoa viwanja, yaani kiwanja kimoja kugaiwa mara mbili.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya huyo alisema kuwa rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Iringa hapo tarehe 26.06.2018.
Alisema kuwa rais Magufuli alivutiwa na mapokezi makubwa siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment