Monday, 21 May 2018

MWENGE KUZINDULIWA MIRADI 40 WENYE THAMANI SHILINGI BILIONI 24.42


(Picha na Friday Simbaya)

IRINGA: Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 unatarajia kuzindua jumla ya miradi ya maendeleo 40 yenye thamani ya shilingi billioni 24.42. 

Akiongia na waandishi wa habari jana Mkuu wa Mkoa wa iringa Amina Masenza alisema kuwa miradi hiyo inatoka sekta za elimu kumi (10), afya saba (7), maji nne (4), malisali moja, kilimo tano (5), viwanda viwili, uvuvi moja, na mapambano dhidi ya rushwa nne (4). 

Alisema kuwa gharama za miradi hiyo zimetokana na michango ya wananchi shilingi bilioni 1.3, serikali kuu shilingi bilioni 8.64, halmashauri shilingi million 253.6 na wadau wa maendeleo shilingi 14.3. 

Masenza alisema kuwa mkoa wa iringa utaanza mbio za mwenge wa uhuru tarehe 23/05/2018 baada ya kuupokea Mkoa wa Mbeya. 

“Ukiwa mkoani Iringa, Mwenge wa Uhuru utapitia kwenye halmashuari zote tano (5) kuhimiza shughuli za maendeleo kama ifuatavyo; halmashauri ya wilaya ya Mufindi tarehe 23/05/2018, halmashauri ya wilaya ya Iringa (24/05/2018), halmashauri ya wilaya ya Kilolo (25/05/2018), halmashauri ya Manispaa ya Iringa (26/05/2018) na halmashauri ya mji Mafinga tarehe 27/05/2018,” Masenza alifafanua. 

Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 zilizinduliwa mkoani Geita na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 02/05/2018 ambao utakimbizwa katika mikoani 31 na hatimaye kuhitimishwa rasmi na Dkt. John Pombe Magufuli huko mkoani Tanga tarehe 14/10/2018. 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...