Saturday, 23 June 2018

ASILIMIA 80 YA AJILI ZINAZOTOKEA NCHINI USABABISHA NA MAKOSA YA KIBINADAMU


Na Friday Simbaya, Iringa 

Hali ya usalama barabarani nchini imekuwa siyo nzuri na hivyo kugharimu maisha ya wananchi kwa kusababisha ajili ambazo zimekuwa na athari ya kusababisha ulemavu na vifo, imefahamika. 

Hayo yalisemwa jana na mkuu wa wilaya ya iringa Richard Kasesela wakati mafunzo ya usalama barabarani, usimamizi wa mazingira na masuala ya kijamii kwa wataalamu wa Tanroads yanayendelea kufanyika mkoani Iringa. 

Mafunzo hayo siku nne ni kwa ajili ya kukuza weledi wa wafanyakazi wa TANROADS katika kutatua changamoto wakati kutekeleza miradi ya barabara. 

Mkuu wa wilaya huyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa iringa Amina Masenza, alisema kuwa ilikupunguza matatizo hayo wakala wa barabara nchini (TANROADS) wanatakiwa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wananchi na hata kwa wafanyakazi wake katika kutambua maeneo hatarishi. 

Alisema kuwa baadhi ya sababu zinazosababisha ajali ni pamoja na makosa ya kibinadamu ambayo huchangia asilimia 80, ubovu wa barabara unachangia asilimia nane (8%) na ubovu wa magari ambao unachangia asilimia 12. 

Kasesela alivitaja vyanzo vikuu vya ajili kuwa ni pamoja na mwendokasi wa madereva, kulipita gari linguine kwenye mlima au kona kali, kutoheshimu alama za barabarani, utumiaji wa barabara sio zingatia sheria, kukosekana kwa alama za barabara ambazo huibwa au kugongwa na magari na kukusekana kwa michoro ya barabarani. 

Kwa upande wa usimamizi wa mazingira, alisema pia hali siyo nzuri sana kwa vile wadau wengi wamekuwa hawaoni umuhimu uliopo katika usimamizi wa mazingira kwa utekelezaji wa miradi ya barabara. 

“Ni mara nyingi sana kukuta mkandarasi anachimba kifusi au kokoto kwa ajili ya ujenzi wa barabara na kuaacha mashimo bila kuyarekebisha ili kupunguza athari zinazo weza kutokea kwa kuwepo mashimo hayo,” alisema Kasesela. 

Aidha unapotembelea barabara zetu utakuta takataka mbalimbali ambazo zimetupwa na wasafiri barabarani na wakati mwingine wasfiri kujisaidia ovyo pembezoni mwa barabara maarufu kama ‘kuchimba dawa,’ alisema. 

Pamoja na kuwepo matatizo mengi ya usimamizi wa mazingira katika utekelezaji wa miradi ya barabara, wataalumu wa TANROADS wanatakiwa kujengewa mikakati ya kuyapunguza. 

Katika masuala ya kijamii kumekuwa na changamoto za ukimwi, usalama na afya mahali pakazi na kuhamisha watu katika hifadhi ya barabara. 

Kasesela alisema kuwa changamoto hizo bila kuziwekea mikakati madhubuti zitaleta athari kubwa kwa jamii katika utekelezaji wa miradi ya barabara. 

Kwa upande wake, mkuu wa idara ya mazingiara na usalama TANROADS makao makuu Zafarani Madayi alisema kuwa mafunzo hayo ni utaratibu wa kawaida ambao tanroads imejiwekea kila mwaka. 

Alisema lengo kubwa la warsha hizo za kila mwaka ni kujenga weledi kwa watumishi wake katika kusimamia na kutekeleza masuala ya mazingira, kijamii na usalama barabarani. 

Madayi alisema hayo ni masuala mtambuka yanayokwnda sambamaba na utekelezaji wa miradi ya barabara kuu na za mikoa nchini. 

Alisema kuwa kwa kawaida mafunzo hayo hutolewa kikanda na sasa ni zamu ya kanda ya nyanda za juu kasini ambapo mkoa wairinga ndio mwenyeji. 

Madayi aliongeza kuwa warsha hiyo imejumisha washiriki kutoka TANROADS makao makuu na ofisi za TANROADS mikoa yote 26 nchini. 

Washiriki hao ni wataalumu w tanroads wanaohusika na masuala ya mazingira, usalama barabarani, kijamii/UKIMWI, utunzaji wa hifadhi ya barabara, usanifu, ujenzi na matengezo ya barabara, ukaguzi wa mahesabu, rasilimali watu, madereva, na wataalumu wengine. 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...