Shirika la kuwasaidia watoto wa kike-CAMFED TANZANIA, wilaya ya Iringa limesaidia wasichana 76 kujiunga na elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini katika kipindi cha mwaka 2017/2018.
Shirika la Camfed linasaidia wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi kidado cha sita na hatimaye kujiunga elimu ya juu kwa wasichana wanaotoka katika familia duni kwa lengo la kuwakwamua na umasikini.
Mratibu wa miradi ya Camfed Wilaya ya iringa, Abia Mwisaka alisema hayo wakati ya kongamano la wasichana wanaosoma katika vyuo mbalimbali lililoandaliwa na shirika hilo mkoani Iringa jana.
Alisema kuwa wasichana hao walisaidiwa na shirika hilo kuendelea na elimu ya juu katika vyuo mbalimbali vilivyopo mikoa ya Sumbawanga, Njombe na Iringa.
Mwisaka alisema kuwa lengo la kongamano hilo lilikuwa kwa ajili kuangalia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wasichana walioko vyuoni ili kuona namna gani wanaweza kuepukana nazo.
Alisema kuwa katika kongamano hilo pia waliwaalika wataalam mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia katika Nyanja mbalimbali za maisha pamoja na namna gani wanaweza kuishi wakati wakiwa vyuoni ili kuepukana na hizo changamoto.
Wataalamu walioalikwa kwenye kongamano ni pamoja na mtaalam wa afya ambaye aliwapitisha katika mambo ya afya kama vile namna ya kujikinga na VVU/UKIMWI, adhari za ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni.
Alisema kuwa wasichana wakiwa katika afya njema wataweza kujikinga na kutimiza ndoto zao za kusoma na baadaye kupata ajira kwa vile wasichana wengi wanatoka katika mazingira tofauti, yaani wengine wanatoka maeneo ya vijijini, kwayo wasipopewa elimu ya afya wanaweza kushindwa kutimiza malengo yao.
Pia, alisema kuwa wasichana hao wakiwa katika kongamano hilo walipitisha katika sera ya ulinzi wa mtoto ili kuwajuza juu ya ulinzi wa mtoto kuhakikisha mtoto analindwa na kuheshimiwa.
Mwisaka alisema wataalamu wengine walioalikwa ni pamoja na afisa utumishi wa Wilaya ya Iringa aliyewapitisha wasichana hao katika namna ya kuandika CV nzuri, kuandika barua ya kazi na vitu gani wanatakiwa kufanya wanapoitwa kwenye usaili, ili wamalizapo vyuo wasipate shida.
Mtaalumu mwingine aliyealikwa katika kongamano hilo ni Yule wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi ilikuweza kuwaunganisha wasichana hao na bodi ya mikopo ambaye aliwaeleza namna ya kuomba mikopo na nani anastahili kupata mkopo wa wanafunzi.
Naye, mtaalamu kutoka chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE) Dr. Winston Mdegella waliwataka wasichana hao waiishi maisha yao na sio maisha ya kufuata mkumbo wanapokuwa vyuoni.
Alisema kuwa maisha ya chuo ni maisha yanaomwezesha mtu kijitafakari na kujitambua tofuati na maisha ya shule ya msingi na sekondari.
Dr. Mdegella alisisitiza kuwa maisha ya chuo ni maisha huru lakini uhuru huo usiutumie vibaya ambao mwisho wake unamadhara mengi kuliko faida.
Aliwaasa wasichana na wanafunzi wengine kusoma kwa bidii kwaani asilimia 80 waielekeze katika masomo na asilimia 20 iliobaki ndio wawezetumia kwa mambo mengine.
Kwa upande wake, Ofisa Elimu wa Wilaya ya Kilolo, Gloria Kang’omba waliwataka wasichana hao kufikilia nje ya boski kwa kuwa ajira kwa sasa zimekuwa za shida lakini waelekeze mawazo yao katika kujiajiri.
Alisema kuwa wasichana hao wanatakiwa kusoma kwa bidii liwaweze kufanya vizuri katika masomo yao na hatimaye kukuwa katika soko la ajira.
Kang’omba alisema kuwa wanafunzi wanaomaliza vyuo nchini ni kubwa na kila mwaka wanafunzi mbalimbali katika vyuo ni wengi kwa hiyo wasichana hao wanabudi kufikilia kujiari kulikokuajiriwa.
Wakati huohuo, Ofisa mikopo kutoka chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE) Dr. Kennedy Muhema akitoa taarifa ya bodi ya mikopo wanafunzi alisema kuwa bodi hiyo tangu mwaka 1994/1995 hadi 2017/2018 imeweza kutoa mikopo kwa wanafunzi 438,257 wenye thamani ya trillion tatu (3trn/-).
Alisema kuwa katika mwaka wa masomo 2017/2018 bodi hiyo imepanga kuwapatia mikopo wanafunzi wapatao 120,417 kati yao 33,857 ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza na 86,560 ni wanafunzi wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali nchini.
Dr. Muhema pia alisema kuwa katika mwaka wa masomo 2018/2019 inatajiwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wapatao 124,000 ambapo kati yao 40,544 ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Na Friday Simbaya, Iringa
No comments:
Post a Comment