Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkabidhi kompyuta Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William kwa ajili ya kuboresha zoezi la uandaaji na uingizaji wa takwimu za elimumsingi kupitia mfumo wa Tehema wa basic education management information system (BEMIS), zilizotolewa na ofisi ya Rais-/Tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya elimu, sayansi na teknolojia jana.(Picha na Friday Simbaya)
|
Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma ya elimu nchini imeaanza kutoa vifa vya tehema kwa ajili ya kuboresha zoezi la uandaji na uingizaji wa takwimu za elimumsingi kupitia mfumo wa BEMIS (basic education management system).
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema hayo jana wakati wa kukabidhi vifaa vya tehema na samani kwa Mkuu wa Wilaya wa Mufindi Jamhuri William vilivyotolewa na Ofisi ya Rais-Tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.
Alisema kuwa takwimu sahihi ni muhimu sana katika kuiwesha serikali kuweka mipango mbalimabli kwa ajili ya ustawi wa jamii katika huduma za elimu, afya na maji.
Masenza alisema kuwa ili serikali iweze kugawanya rasilimali kwa uwiano unaotakiwa, kiijumla takwimu sahihi ni kila kitu katika kupanga maendeleo ya watu na shughuli zao.
Alisema kuwa vifaa hivyo vitafungwa kwenye ofisi za maofisa elimu vifaana takwimu (SLOs) kwa halmashauri zote nchini na maofisa elimu taaluma kwa ngazi ya mikoa.
Kila mkoa/halmashauri imepatiwa kompyuta tatu (3), printa moja, UPS tatu (3) pamoja na samani ambazo ni meza tatu (3) na viti vitatu (3) kwa ajili ya shughuli za uingiza wa takwimu za elimumsingi.
No comments:
Post a Comment