Tuesday, 7 August 2018

ASILIMIA 42 YA WATOTO CHINI YA MIKA MITANO MKOANI IRINGA WAMEDUMAA



Kikundi cha wazee wa Kilolo cha utamaduni wa kabila la wahehe kikitoa burudani wakati wa Kilele cha maadhimisho unyonyeshaji maziwa ya mama duniani yalioanza tarehe 01-07, August, 2018 yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Kilolo wilayani Kilolo, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)






Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 42 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Iringa wamedumaa, asilimia 3.6 wamekonda na asilimia 13.8 wana uzito pungufu ukilinganisha na umri wao. 

Akizungumza na mganga mkuu wa mkoa wa iringa (RMO), Dr. Robert Salim kwa nia ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi wakati wa siku ya killele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwaya mama duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijii cha Kilolo wilayani Kilolo, mkoani iringa jana. 

Alisema kuwa unyonyeshaji watoto maziwa ya mama unafaida nyinyi kwa upande zote mbili kwa mtoto anayenyonya maziwa na mama anayenyonyesha. 

Hapi alisema kuwa kwa mtoto anayenyonya maziwa ya mama ndiyo chakula pekee kinachompatia virutubishi vyote anavyohitaji kwa uwiano sahihi kwa afya na ustawi. 

Aliongeza kuwa maziwa ya mama ndiyo chakula pekee chenye viini vya kingamwili ambavyo hufanya kazi kama chanjo inayomlinda mtoto dhidi ya maradhi na kumsaidia kuhimili maradhipindi anapopata maambulizi mbalimbali. 

Hapi alisema kuwa faida nyingine ni kwamba maziwa hayo ya mama humeng’enywe na kufyonzwa kwa urahisi zaidi mwa mtoto ukilinganisha na vyakula akue na apate maendeleo mazuri kimwili na kiakili. 

“Mtoto anayenyonyeshwa ipasavyo huongezaka urefu kulingana na umri kwa kasi nzuri hali inayomfanya awe na kiwango kizuri cha uelewa wa mambo yanayomzunguka,” alisisitiza. 

Alisema kuwa hali hii huchangia kupata alama nzuri katika masoso yake darasani na kuongeza kuwa unyonyenyeshaji wa maziwa ya mama unaupatia nguvu mfumo wa ukuaji na maendeleo ya ufahamu na utambuzi (IQ)wa mtoto. 

Hivyo, kwa kiasi kikubwa husaidia katika kuimarisha mannikio ya elimu, ushirika katika nguvu kazi na kuongeza kipato katika maisha ya baadaye ya mtoto. Na Friday Simbaya, Kilolo 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...