Na Friday Simbaya, Iringa
Jeshi la polisi mkoani iringa inamshikilia mama mmoja kwa tuhuma ya kumtumikisha kingono binti yake mwenye miaka 14 kwa lengo la la kujipatia kipato na pindi akaapo humpiga.
Akizumgumza na wanahabari mkoani Iringa jana Kamanda wa Polisi mkoani Iringa ACP Juma Bwire alisema tukio hilo lilitokea tarehe 02.08.2018 majira ya saa 4 asubuhi huko maeneo ya Mwangata, Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo Dina Juma,45 mkazi wa Mwangata kwa majira tofauti alikuwa akimtumikisha kingono mtoto wake jina limehifadhiwa mwenye umri ya miaka 14 kwa lengo la kujipatia kipato.
Kamanda Bwire alifafanua kuwa uchunguzi wa dakatari umethibitisha kuwa binti huyo alifanyiwa vitendo hivyo muda mrefu ambapo tarehe 03.08.2018 amefanyiwa vitendo hivyo na mtuhumiwa alipiga kwa kumshurutisha.
Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi unaendelea lakini mtoto amehifadhiwa ustawi wa jamii kwa uangalizi kutokana na kuwa na matatizo ya akili.
Wakati huohuo, jeshi la mkoa wa Iringa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma ya kutorosha wanafunzi kwenda kufanya kazi za ndani.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa ACP Juma Bwire alisema mnamo tarehe 31.07.2018 majira ya saa 4:30 asubuhi huko katika mji mdogo wa Ilula, tarafa ya Mazombe wilayani Kilolo, mkoa wa iringa wamewakata watuhumiwa wawili walipokuwa wakihangaika kuwasafirisha wanafunzi watano wa sekonadri ya Mlafi kwenda Dar es Salaam kufanya kazi za ndani.
Wanafunzi hao walitoweka kwa wazazi wao tangu 29.07.2018 majira ya saa 12 jioni na kusafirishwa kwa bodaboda kutoka Mlafi hadi Ilula na watuhumiwa hao.
ACP Bwire aliwataja watuhimiwa hao kuwa ni Tulizo Mtega,19, na Rosemary Msasalage,18, wote wakazi wa Ilula na kuogeza kuwa binu iliyotumika ni kuwarubuni wanafunzi hao kuwa watapata kazi mbalimbali za kuuza maduka Morogoro na Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment