Na Friday Simbaya, Mufindi
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau wa haki za watoto kutunga sheria kali dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyochangia watoto kushindwa kutimiza ndoto zao.
Wakizungumza jana wakati wa semina wa mabaraza ya watoto ngazi ya kata wanafunzi hao wanasema vitendo vya ukatili vimekuwa vikiongezeka kila siku kwa jamii inayo wazunguka kutokana na kutokuwapo kwa sheria kali dhidi yao huku wazazi wakionekana kushindwa kutimiza haki za watoto.
Malezi mabaya ya familia yanachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vitendo viovu ikiwamo ubakaji na ulawiti hivyo Wazazi ,walezi na jamii kwa ujumla wanayonafasi kubwa ya kuijenga jamii yenye maadili dhidi ya vitendo viovu.
Jumla ya watoto 140 kutoka kata za Bumilinyinga, Idunda na Ihowanza walishirika semina ya baraza la watoto ngazi ya kata kuhusu ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Asasi isiyoyakiserikali ya SOS Children’s Villages Tanzania kwa shirikiana na Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.
Mmoja wa wajumbe wa baraza la watoto toka kata ya Ihowanza, Evelina Mwilapwa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Ihowanza alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inapaswa kutunga sheria kali itakayoza kudhibiti viovu dhidi ya watoto.
Alisema kuwa serikali kuwa serikali inatakiwa kulitilia umuhimu suala la ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike ambao wana kumbana nalo kuanzia ngazi ya familia hadi jamii.
Mwilapwa alisema kuwa wapo wazazi na walezi wenye mtazamo hasa juu ya watoto wakike kwa kuwanyimwa fursa ya kupata elimu pamoja na kubaguliwa.
Ofisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Navoneiwa Mfinanga alisema licha ya kutoa elimu kwa wazazi bado changamoto ya ukatili kwa watoto imeonekana kukithiri miongoni mwa wazazi na walezi huku akieleza mikakati ya serikali juu ya jambo hilo.
Alisema kuwa changamoto za ukatili wa kijinsia umeanza kupungua kutokana na elimu ya ukatili wa kijinsia kwa jamii kupitia kamati mbalimbali mazingira hatarishi.
Mfinanga alisema kuwa yeye kama mratibu wa mabaraza ya watoto wamefanyikiwa kuunga mabaraza ya watoto ngazi ya kijiji,kata na ngazi ya wilaya.
Aidha, ofisa maendeleo ya jamii aliyeshiriki kuendesha semina kwa watoto wa mabaraza ya watoto ngazi ya kati ni Grace Kalomeji toka halmashuri ya mji mafinga, wilayani Mufindi.
Kokutona Kayungi ni Ofisa Mradi wa Shirika la SOS Children’s Villages Tanzania wilayani Mufindi kupitia mradi wa kuwezesha wanawake kiuchumi na haki za watoto alisema kuwa semina hiyo walikuwa ni kuimarisha na kuyajengea uwezo mabaraza ya watoto ili wawezekutambua haki zao ili waweze kupaza sauti zao juu ya masuala ya ukatili wa kijisia.
Alisema kuwa kupitia mabaraza ya watoto ni jukwaa la watoto ambapo wanajadili mambo yao yanayowahusu wao wenyewe hasa ubakaji, mimba za utotoni pamoja na wawake kutopewa haki ya kumiliki mali.
kayungi pia alisema ukalitili ya kijinsia mara nyingi utokea katika ngazi ya familia kwa kupitia mabaraza hayowa watoto wanafundishwa namna ya kutambua haki za ilikuweza kuripoti vitendo vya ukatili katika madawati ya kijinsia ambayo hapo katika maeneo yao.
Aliongeza kuwa Asasi ya SOS childrens Villages Tanzania pia inatoa mafunzo ya kujenga uwezo wa walezi wa watoto, familia zao na jamii ili watoto wapate malezi ya kutosha.
Kayungi alisema kuwa watoto takribani 140 toka kata za Bumilinyinga, Idunda na Ihowanza wamekutana kupitia mabaraza ya watoto yaliyopo Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kubadilishana mitazamo na kupaza sauti kwa mambo yanayowahusu.
“Watoto hawa kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi za vitendo vya ukatili kama kubakwa, ndoa za utotoni pamoja na kufanyishwa kazi ngumu na katika siku za hivi karibuni,” alisema.
Mwisho