KESI ya kutoa hongo katika mchakato wa kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Mufindi Kaskazini na Waziri katika serikali za awamu zote nne, Joseph Mungai imetajwa tena leo (Agosti 25) katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa.
Mungai (66) pamoja na makada wengine wawili ambao ni Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM wa Wilaya ya Mufindi, Fidel Cholela (39) na Moses Masasi wanakabiliwa na mashtaka 15 ya rushwa kinyume na sheria ya kuzuia na kupamna na rushwa ya mwaka 2007 na sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 .
Watuhumiwa hao kwa pamoja, kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Agosti 11, mwaka huu na kusomewa mashitaka hayo ambayo pia waliyakana.
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa, Marry Senapee, ambapo upande wa mashitaka uliokuwa ukiongozwa na Prisca Mpeka kutoka Takukuru, uliomba tarehe nyingine ya shauri hilo kwa ajili ya kusoma maelezo ya awali yanayoweza kuruhusu kuanza kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, Wakili anayewatetea washitakiwa hao, Basil Mkwatta aliomba tarehe itakayopangwa na mahakama hiyo alete pingimizi la awali la kisheria kwamba kesi hiyo haistahili kuwepo mahakamani hapo.
Pande zote mbili zilikubaliana ambapo Hakimu Senapee alipanga kesi hiyo irejeshwe mahakamani hapo Septemba 30 mwaka huu ambapo Mkwatta ataleta pingamizi hilo na hivyo kumfanya mwendesha mashitaka wa Takukuru,Prisca Mpeka asisome maelezo ya awali siku hiyo na badala yake atalazimika kusubiri kusikia pingamizi hilo na kutoa hoja za kujibu.
Inadaiwa kuwa Julai 08, mwaka huu, katika kata ya Ihalimba, Wilaya ya Mufindi, Mungai akiwa mmoja wa makada wa CCM waliokuwa wanawania kupitishwa katika kura za maoni kugombea ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, kwa pamoja na watuhumiwa wenzake, walitoa hongo ya Sh.10,000 kwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Vikula kama kishawishi cha kumpigia kura wakati wa zoezi la upigaji wa kura za maoni.
Katika shtaka la pili, inadaiwa kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja, siku na katika eneo hilo walitoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Konjesta Kiyeyeu ambaye alihudhuria kikao cha kamati ya CCM Kijiji cha Vikula.
Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa, katika shtaka la tatu, nne, tano na sita, watuhumiwa wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Aldo Lugusi, Ezekiel Mhewa, Tulaigwa Kisinda na Jiston Mhagama kwa lengo hilo hilo la kuwashawishi wampigie kura za maoni.
Katika shitaka la saba,watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.20,000/- kwa Maria Kihongosi na shtaka la nane kutoa hongo ya Sh.5,000/- kwa Lurent Mdalingwa wakati shtaka la tisa wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.20,000/- kwa Victory Kalinga ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Kijiji cha Ugessa.
Katika mashtaka namba kumi hadi 12 washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa walitoa hongo ya Sh.2,000/- kwa Francis Chonya, Alfred Kisinga na Issac Tewele wakati shtaka la 13 wanadaiwa walitoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Sosten Kigahe.
Aidha, Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa shitaka namba 14 watuhumiwa wanadaiwa kutoa hongo ya Sh.10,000/- kwa Raphael Lutumo na shitaka la mwisho walitoa hongo ya Sh.20,000/- kwa Andrew Mkiwa.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...
No comments:
Post a Comment