Monday, 16 August 2010
VIKAO VYA MAHAKAMA RUFANI
OFISI ya Mkurugenzi mkuu wa mashitaka nchini (DPP), imeiondoa rmahakamani rufaa iliyokata kwenye mahakama ya rufaa ya Tanzania, dhidi ya Philbert Mtweve aliyeomba rushwa ya sh. 15,000 kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kennedy Rubindu.
Wakili wa serikali, Vicent Tangoh, aliomba kuondoa rufaa hiyo kupitia kanuni ya 4(ii)(a) ya mwaka 2009 ya mahakama ya rufaa, mbele ya majaji watatu waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo, Edward Rutakangwa, Natalia Kimaro na William Mandia.
"Awali tuliwasilisha taarifa ya kuondoa rufaa hii kwa kanuni ya 77(i) na tukagundua kanuni hiyo sio sahihi kuitumia kwani inaeleza kuondoa rufaa kwa msajili na sio mahakama ya rufaa, hivyo sasa tunaomba kwa kupitia kanuni ya rufaa kuondoa rufaa hii," Tangoh aliwaeleza majaji hao mahakamani hapo.
Baada ya ombi hilo, Jaji Rutakangwa alishauriana na wenzake na kukubaliana na ombi hilo na kuamua kuondoa rufaa hiyo iliyokuwa imekatwa na DPP.
Awali mwaka 2001, Mtweve alidaiwa na mahakama ya Wilaya ya Mbinga kuwa alichukua rushwa ya sh. 15,000 kutoka kwa Rubindu aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi ili amsaidie kumhamishia katika shule ya maeneo ya karibu na wazazi wake.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimuachia huru Mtweve baada ya kukosekana ushahidi lakini serikali kupitia makahama kuu walikata rufaa na Jaji Manento alitoa uamuzi mwaka 2002 wa kuona mshtakiwa hana hatia na baadaye DPP tena akakata rufaa kwenye mahakama ya rufaa Tanzania kupinga maamuzi hayo, lakini mwanasheria wake ameondoa rufaa hiyo mahakamani.
Wakati huohuo,Rufaa ya Yassin Thomas wa Songea ya kupinga kunyongwa hadi kufa iliyotolewa mwaka 2007 baada ya kumuua Mwanaidi Abdallah mwaka 2004, iliyokuwa isikilizwe leo kwenye mahakama ya rufaa ya Tanzania iliyoketi Iringa imesogezwa mbele hadi Ijumaa (Agosti 20), baada ya wakili wa kujitegemea, Basil Mkwata kuomba ili aweze kupitia sababu za rufani hiyo.
"Mwenyekiti, nilikuwa Dodoma katika kikao cha nusu mwaka cha mawakili na nikiwa njiani kurudi nikaambiwa nipitie hapa kuna rufaa na sijapata muda wa kupitia faili la kesi hii, naomba ipangwe siku nyingine ili niweze kusoma sababu za rufaa," aliomba Mkwata kwa Mwenyekiti wa jopo hilo la majaji.
Hatahivyo wakili wa serikali Michael Lwena alipendekeza isikilizwe Agosti 27, lakini Jaji Rutakangwa baada ya kujadiliana na wenzake walipanga kuwa Ijumaa, huku akimtaka wakili huyo kuhakikisha anasoma sababu hizo kwani ameahirisha kwa shingo upande kutokana na mahakama hiyo kuwa na rufaa nyingi zisizotoa muda wa mapumziko.
Mahakama hiyo iliyoanza jana inajumla ya rufaa 30 ambazo za jinai ni 24 na zilizobaki ni za madai na inatarajiwa kumalizika Septemba 6.
MWISHO
*****
UPUNGUFU wa majaji wa mahakama ya rufaa ya Tanzania unasababisha rufaa nyingi kuchukua muda mrefu kusikilizwa na kutolewa maamuzi, imeelezwa.
Naibu Msaijili wa mahakama ya Rufaa Tanzania, John Mgetta alibainisha hayo leo mara baada ya kikao cha kusikilizwa rufaa zilizokatwa na pande mbalimbali wakipinga maamuzi ya mahakama kuu, kilichokaa Iringa na kujumuisha pia rufaa za Songea.
Mgetta alisema majaji hao wapo 16 pekee ambapo wanatakiwa kujigawa katika kanda 10 huku Dar es Salaam ikiwa na majaji sita tofauti na kanda nyingine ambao ni watatu pekee.
Alisema majaji hao 16 wanatakiwa kutoa maamuzi katika kanda za Arusha, Dodoma, Tanga, Mbeya, Sumbawanga, Mwanza, Tabora, Mtwara, Dar es Salaam na Iringa.
Alitoa mfano wa Kanda Iringa inayokaa mara moja kwa mwaka ikijumuisha rufaa za Iringa na Songea rufaa zake zimeanza jana ambazo zipo 30 na zinasikilizwa na majaji watatu, Edward Rutakangwa, Natalia Kimaro na William Mandia na zitamalizika Septemba 6.
"Angalia mtu kakata rufaa tangu mwaka 2008 mwaka huu ndo inaanza kusikilizwa na hii ni sababu ya majaji wachache kwani kama wangekuwa wengi ingekuwa imeshaisha," alisema Mgetta.
MWISHO
*****
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment