Katika Jimbo la Ismani, ni mgombea mmoja tu ambaye ni Bw. William Lukuvi (CCM) ndiye karudisha fomu ya uteuzi kati ya wagombea watatu waliochukuwa fomu pamoja na Bw. Joseph Kapwani (CHADEMA) na Bw. Juma Fufumbe (CUF).
Bw. Lukuvi atatangazwa mshindi wa bila kupingwa katika Jimbo la Isimani baada ya maasa 24 na Msimamizi wa Uchaguzi, Bi. Tina Sekambo wa Wilaya ya Iringa, baada ya wagombea wengine kutorudisha fomu zao kabla ya saa 10 jioni.
Katika Jimbo la Kalenga, waliochukuwa fomu walikuwa wanne na wote wamerudisha fomu zao kabla ya muda uliopangwa na tume ya uchaguzi (NEC).
Waliochukuwa fomu za uteuzi na kurejesha ni pamoja na Bw. Katindasa Lumunko (TLP), Dkt. William Mgimwa (CCM), Bw. Makuke Majinga (Jahazi Asilia)na Bi. Rehema Paulo (CHADEMA).
Katika jimbo la Iringa Mjini ambapo aliyekuwa mshindi katika kura za maoni mwanzoni mwa mwezi huu, Bw. Frederick Mwakalebela ambaye pia ayeeuenguliwa NEC ya chama cha CCM baada ya kashfa ya kutoa rushwa na kesi yake inaendelea mahamani, na kumteuwa mshindi wa pili Bi. Monica Mbega kupitia tiketi ya CCM, basi urejeshaji wa fomu za uteuzi za ubunge umekamilika vizuri leo.
Bw. Willam Lukuvi akiongea na wana habari leo baada ya Msimamizi wa Uchaguzi katika Wilaya ya Iringa Bi. Tina Sekambo kumaliza kubandika fomu za uteuzi ubaoni.Mchungaji Peter Msigwa akirudisha fomu ya uteuzi leo kwa msafara wa gari mjini Iringa.
Waliochuwa na kurudisha fomu katika jimbo la Iringa mjini ni pamoja na Bi. Monica Mbega (CCM), Bi. Mariam Mwakingwa (NCCR-Mageuzi), Bi. Zaituni Mwaibula (CUF) na Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA).
No comments:
Post a Comment