Sunday, 1 August 2010
WALIMU WAKOPESHWA PIKIPIKI
Na Friday Simbaya,
Iringa
CHAMA cha Ushirika cha Akiba na Kukopa cha Walimu wa Iringa Vijini na Kilolo (IRTS-SACCOS LTD) kimekabidhi pikipiki kwa walimu wanachama 19 katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya chama hicho jana.
Pikipiki hizo 19, zilitolewa kwa walimu 19 kati ya 27 walikubaliwa kupewa na juhudi zaidi zinafanyika kupata pikipiki nyingine nane (8) zilizobaki ili walimu hao nao waweze kupewa mapema.
Akikabidhi pikipiki kwa walimu, Afisa Elimu wa Wilaya shule za msingi (DEO), William Mkagwa, kwa niaba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa (DED), Tina Sekambo, alisema kuwa amefurahishwa na juhudi za SACCOS ya kutatua matatizo ya usafari kwa walimu wanachama kwa kutoa mikopo ya pikipiki ambazo zitarahisisha sana usafari kutokana na hali ya jiografia ya Wilaya.
Aidha, Sekambo alishauri pia utaratibu wa mikopo ya vyombo hivi uwe endelevu ili hatimaye walimu wote waweze kupata vyombo hivi.
“Ningependa pia nizungumza suala la mikopo, wafanyakazi wengi wamekuwa na tabia ya kukopa katika taasisi mbalimbali zaidi ya mkopo mmoja kwa wakati, ni vizuri ukamaliza mkopo huu wa pikipiki kabla ya kukopa kwingine, kwani mwisho wa siku familia itapata maisha magumu sana pale mfanyakazi anapokuwa hana cha kupeleka nyumbani mwisho wa mwezi,” alisema.
Aliongeza kuwa vyombo hivi vikitumiwe vizuri kwa sababu vinaweza kuwa kichocheo cha kuinua taaluma na maisha ya walimu katika wilaya.
Lakini vyombo hivyo vya usafari vikitumika vibaya vinaweza kuleta madhara makubwa kwa walimu na hatimaye kurudisha nyuma juhudi za wizara katika kutoa elimu bora kwa watoto na kubadilisha maisha ya walimu.
Katibu wa SACCOS, John Mfalamagoha alisema kuwa chama kilianzishwa mwaka 1997 hadi kufikia tarehe 30/07/2010 chama kilikuwa na jumla ya wanachama 1,197 kati yao wanaume ni 564 na wanawake ni 633.
Alisema kuwa walimu waliomba mkopo ni 27 wakiwamo wanaume 20 na wanwake saba (7) lakini walikabidhiwa ni wanaume 12 na wanawake saba jumla 19, na utaratibu wa kupata pikipiki zilizobaki unaendelea kufanyika na zikipatikana wakati wowote zitakabidhiwa kwa waliomba.
Aidha, katibu huyo alisema, malengo ya chama yalikuwa kutoa mkopo wa pikipiki 50 kwa mwaka 2010 lakini waombaji hawakujitokeza kwa wengi na hivyo kufanikiwa kupata waombaji waliokabidhiwa pikipiki jana.
Takwimu zinaonyesha kuwa watu waliopoteza maisha kutokana na ajali za pikipiki nchini mwaka 2010 181 kati ya jumla ya ajali 1,414 zilizotokea. Pia takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 16 ya ajali ya 30,836 za ajali zilizotokea mwaka 2009.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment