Na. Friday Simbaya,
Ludewa
JUMLA ya miradi sabini na moja (71) yenye thamani ya shilingi 8,369,893,729 itakaguliwa, kuzinduliwa, itafunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi mkoani Iringa kwa mwaka 2010 wakati wa mbio za mwenge.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa Iringa Bibi. Gertrude Mpaka juzi wakati akisoma taarifa fupi ya mkoa wa Iringa wakati wa kupokea mwenge wa uhuru mwaka 2010 katika kijiji cha Kipingu, kata ya Manda wilayani Ludewa ukitokea mkoani Ruvuma.
Bi.Mpaka alisema miongoni mwa fedha hizo, shilingi 2,890,484,593 ni fedha toka Serikali kuu, shilingi 951,705,586 ni michango ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa, thamani ya nguvu kazi ya wananchi ni shilingi 1,557,402,245, shilingi 1,413,904,000 ni michango ya watu binafsi na shilingi 1,556,397,305 ni michango ya wahisani na taasisi mbalimbali za maendeleo .
Mwenge wa uhuru mwaka huu unaongozwa na ujumbe usemao “Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na Malaria”
Katibu tawala mkoa alielezia kuwa mapambano dhidi ya Ukimwi yanaendelea kwa kasi mkoani Iringa, na mkoa kwa kushirikiana na asasi za kitaifa na kimataifa na tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) umetekeleza mpango maalumu wa miaka minne wa kupambana na tatizo la Ukimwi ambapo utekelezaji wake ulianza Oktoba, 2008 na utamalizika Septemba 2012 .
Ameyataja maeneo makuu kuwa ni; kuhakikisha upatikanaji wa kutosha na kuendelea kutoa elimu ya juu ya matumizi sahihi ya kondomu, kupeleka karibu na kuboresha huduma za afya kwa jamii ambapo katika kipindi cha 2008/ 2009 jumla ya vituo 35 vya kupima virisi vya Ukimwi na kuto ushauri nasaha (CTC) vimeboreshwa kwa kufanyiwa ukarabati na samani.
Aidha wataalam 227 wamepatiwa mafunzo rejea kuhusu virusi vya Ukimwi na ushauri nasaha na jumla ya wagonjwa 51,137 walifikiwa na huduma za kupima virusi vya Ukimwi na kupata ushauri nasaha (CTC).
Eneo jingine amelitaja kuwa ni kuzijengea uwezo jamii wa kupambana na mila na desturi hatarishi zinazochangia ongezeko la maambukizi mapya ya VVU. Pia kuboresha huduma za magonjwa ya zinaa ambapo katika kipindi cha mwaka 2008/ 2009 kulikuwa na jumla ya vituo 293 vinavyotoa huduma ya magonjwa ya zinaa, wataalamu 288 walipatiwa mafunzo rejea ya huduma za matibabu ya magonjwa ya zinaa na watu 7,569 walifikiwa matibabu ya magonjwa ya zinaa.
Bibi. Mpaka ameongeza eneo lingine kuwa ni kuongeza elimu na uhamasishaji juu ya masuala ya ngono salama kwa makundi yaliyo katika mazingira atarishi ambapo katika kipindi cha mwaka 2008/2009 jumla ya mikutano 395 ya uhamasishaji katika ngazi mbalimbali za jamii ilifanyika, aidha vikundi 181 vya kijamii vilishiriki na jumla ya vipeperushi na mabango 23,000 vya kuelimisha jamii.
Wakati huohuo katika mbio zake zilizoanza wilayani Ludewa jana Mwenge wa uhuru umekagua umekagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment