Thursday, 16 September 2010

MAMBO YA LIVYOKUWA KATIKA UZINDUZI WA DARAJA LA MOJA

Wakati wa jua kali na uchovu wa kazi baada ya uzinduzi wa Daraja la umoja linaloziunganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji, Mtangazaji Maarufu wa TBC Taifa (zamani RTD), Bw. Malima Ndelema akipooza uso kwa maji ya Mto Ruvuma katika eneo la Mtambaswala upande wa Msumbiji hivi karibuni.

Daraja la Umoja linalounganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji lenye urefu wa kilometa moja kasoro katika Mto Ruvuma eneo la Mtambaswala ni kivutio cha kipekee katika masuala mazima ya utalii na kukuza ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.


 Ubovu wa miundombinu ya barabara katika maeneo mengi ya vijijini na mijini yanakwamisha maendeleo ya wananchi na nchi yao kiuchumi, eneo hili kama linavyoonekana mbele ya Mto Rufiji eneo la Nangulukulu  Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ni kikwazo kikubwa cha wasafiri wa maeneo ya Kusini mwa Tanzania hasa wakati wa mvua. Msururu wa magari haya ni kielelezo tosha cha hali hiyo.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...