MGOMBEA kiti cha Ubunge Jimbo la Temeke kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abasi Zuberi Mtemvu amewatoa wasiwasi wapangaji wa nyumba za kota zilizopo Temeke mwisho kwa kuwaeleza kuwa zoezi la kuvunjwa kwa nyumba hizo sasa limesitishwa.
Mgombea huyo alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi uliyofanyika katika uwanja wa MjiMpya Kata ya Azimio jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati wa watu.
Akifafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo Mtemvu alisema serikali iliyoko madarakani imejipanga kujenga majengo ya ghorofa katika eneo hilo ambapo ujenzi wake ukikamilika wapangaji wa awali wa kota watapewa umuhimu wa kwanza kufikiriwa katika kupanga kwenye maghorofa hayo.
Alisema si vyema kuanza zoezi la uvunjaji wa kota hizo bila kuzingatia usalama wa wananchi na mali zao katika kipindi cha mpango huo.
Kota hizo zilizopo eneo la Temeke mwisho zilijengwa miaka mingi iliyopita katika mfumo wa familia moja, mbili na tatu hata hivyo nyumba hizo zimeanza kuchoka na hata baadhi yake kuanza kuharibika.
Kwa upande mwingine mgombea huyo aliwataka wanawake wa jimbo hilo kujiunga pamoja na kuunda vikundi vidogo vidogo (VICOBA) ili waweze kupata misaada ya uwendelezaji wa vikundi vyao ili kuondokana na umasikini wa kipato na kuboresha familia zao.
Akizumgumzia huduma za jamii upande wa elimu alisema endapo atachaguliwa tena kuongoza jimbo hilo atahakikisha kuwa kata ya Azimio inapata sekondari ya kidato cha tana na sita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment