Baadhi ya misaada iliyotolewa na jamii ya waislamu kutoka Iringa Mjini na Wilaya ya Iringa vikiwa vinagawiwa kwa wananchi wa Kijiji cha Isimani-Tarafani wilayani Iringa waliyokumbwa na tatizo la chakula kutokana na ukame. Waislamu hao alitoa sembe tani mbili (2), maharage kilo 1,500, mafuta ya kula, sabuni na sukari vyenye thamani ya milioni saba (7m/-).
Mkazi wa Isimani-Tarafani akimsaidia mlevu kusukuma baiskeli iliyoshehena msaada wa chakula bbad ya kupata mgawo.
Mwakilishi wa waislamu waliotoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Isimani-Tarafani wilayani Iringa, Mkoa wa Iringa Bw. Elimi Shams (kulia) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza zoezi la kugawa misaada kwa wananchi waliokubwa na uhaba wa chakula kutokana na ukame.
SHEIKH Sharrif Abdullah Hussein-Kateshi na kiongozi wa waislamu mkoani Manyara (kulia) akibadilishana mawazo na Sheikh wa Tarafa ya Isimani Athumani Hussein Mfilinge (katikati) pamoja na Mwakilishi wa Msafara Elimi Shams (kushoto) leo wakati wa hafla ya ugawaji chakula cha msaada pamoja na mambo mengine kwa wananchi wa Kijiji cha Isimani-Tarafani waliyokumbwa na upungufu wa chakuala kutokana na ukame.
Wakazi wa Isimani-tarafani wilayani Iringa, Mkoa wa Iringa wakiwa wanasubiri kuchukuwa chakula cha msaada kilichotolewa na waislamu kutoka Iringa mjini na Wilaya ya Iringa Jumanne baada ya wakazi hao kukumbwa na upungufu wa chakula kutokana ukame.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment