Thursday, 28 October 2010
VIZIWI HAWAJUI NI CHAMA KIPI CHA KUCHUGUA OCTOBA 31
Na Francis Godwin,
Iringa
HUKU ikiwa zikiwa zimebaki siku mbili pekee ili watanzania wote waliojiandikasha na wenye sifa ya kupiga kura kushiriki katika zoezi la uchaguzi wa Rais ,wabunge na madiwani zaidi ya watu walemavu wa kusikia (Viziwi) 2000 katika mkoa wa Iringa kushiriki uchaguzi mkuu katika mchezo wa bahati nasibu.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi wa habari hizi ndani ya mkoa wa Iringa umebaini kasoro mbali mbali ambazo zimefanywa na wagombea karibu wote wa vyama vya siasa wakati wa kampeni zao baada ya kushindwa kuweka mpango mzuri wa kuwafikia viziwi na jamii nyingine yenye ulemavu katika kunadi sera zao.
Japo kwa upande wa jumuiko la asasi za kiraia Tanzania mkoani kwa mikoa ya Iringa,Mbeya ,Rukwa na Ruvuma zimeweza kwa kiasi chake kuwakutanisha wagombea wa nafasi ya ubunge na makundi mbali mbali ya jamii wakiwemo viziwi ambao hata hivyo wamepata kusikiliza sera za baadhi ya vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) ambao ndio walikuwa hawakosi katika midahalo hiyo huku CCM na baadhi ya vyama hadi sasa hawajapata kukutana na watu hao .
Shaibu Juma ni katibu wa chama cha viziwi Tanzania mkoani Iringa akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa vyama vya siasa vimelisahau kundi la watu hao na kuwa upo uwezekano wa kundi hilo kushindwa kuchagua viongozi bora kutokana na kutofikiwa na wagombea hao katika kampeni zao ili kunadi sera zao.
Alisema kuwa uchaguzi mkuu kwa Tanzania ni uchaguzi wa kidemokrasia ambao kwa mara ya tano sasa unakwenda kushirikisha vyama vingi vya siasa katika nafasi mbali mbali pia ni uchaguzi wenye kuonyesha sura halisi ya demokrasia nchini Tanzania bila kusahau amani ,upendo na utulivu kama ilivyozoeleka kwa nchi za Afrika na dunia kwa ujumla kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani ila hadi sasa upendo kwa viziwi bado haujaonyeshwa.
“Ikumbukwe kuwa kampeni za uchaguzi mkuu wa wabunge,madiwani na Rais zimepata kuanza kitambo kirefu na hadi sasa muda umewadia wa watanzania kuweza kutimiza haki zao za msingi kwa kuchagua Rais,mbunge na diwani…..sasa hadi sasa zaidi ya midahalo ya jumuiko la asasi za kiraia hakuna chama kilichofika kukutana na viziwi kutuomba kura “
Pamoja na kampeni hizi kuaza hadi sasa viziwi wamebaguliwa na kutengwa na uchaguzi huo kwani hakuna mgombea amepata kufika kuomba kura ama kunadi sera za chama chake hivyo ni vigumu kuchagua kiongozi bila kujua atatutumikia vipi .
Wakati chama cha viziwi mkoa wa Iringa kikieleza jinsi ambavyo kinaingia katika uchaguzi mkuu kuchagua bila kujua sera za vyama mgombea ubunge katika jimbo la Mpanda vijijini mkoani Rukwa kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ,Charlesy Makofia alisema kuwa tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC)pia inapaswa kutupiwa lawama zote kwani ilipaswa kutoa maelekezo kwa vyama kupanga ratiba zao za kampeni kwa makundi yote ili kufikiwa na sera za wagombea.
Alisema NEC imekuwa ikieleza jinsi ambavyo walivyoandaa mazingira mazuri ya walemavu kushiriki kupiga kura bila kuweka mpango mzuri wa kuvishauri vyama kuanza kampeni zake kwa kundi la walemavu na kungekuwepo na utaratibu wa kuhakikisha kila mkutano wa kampeni viziwi wanakuwepo na kusaidiwa kuelewa sera za vyama.
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Mary Tesha alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kama chama chake kimeweza kuwafikia watu hao wenye ulemavu ,alisema kuwa kimsingi viongozi wa wilaya ndio ambao walitakiwa kupanga kampeni za kuyafikia makundi hayo na kuwa anamani kuwa wamefanya hivyo japo hakuweza kuthibitisha zaidi.
Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa mkoani Iringa Ismail Makuke ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama cha Jahazi Asilia Tanzania alisema kuwa kuwa kimsingi vyama bado havikuwa na wataalam wa kusaidia kutafsiri lugha kwa viziwi japo baadhi ya walemavu hao wamekuwa wakikutana nao mitaani na kuwaomba kura japo sio kupitia mikutano hiyo.
“Tume ya Taifa ya uchaguzi yenyewe ilisema kuwa kuna vifaa maalum vya kuwawezesha viziwi kupiga kura …..ila bado watakuwa wanashiriki kuchagua viongozi bila kujua sera zao zaidi ya kutazama rangi za bendera na kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya wagombea kukosa kura kama bendera za vyama hazitavutia machoni pa watu hao.
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...
No comments:
Post a Comment