Thursday, 25 November 2010

JK ATEUWA BARAZA LA MAWAZIRI












Rais wa Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete


Katika Muundo wa Serikali hakuna mabadiliko makubwa isipokuwa yafuatayo:


1. Idara ya Umwagiliaji tumeiunganisha na Kilimo ambako ndipo ilipokuwa zamani.


1. Imeonekana upangaji wa maendeleo ya kilimo unakuwa hauna hakika bila ya umwagiliaji kuwa sehemu ya kilimo. Tuliihamishia maji kurahisisha pia upangaji na hasa kwa vile maji ndiyo wanaotoa haki ya matumizi ya maji.


2. Kwa kuwa tatizo la uhaba wa maji ya binadamu ni kubwa sana na tunataka tuongeze kasi ya kukabiliana na tatizo hilo tumeona tuiondolee wizara hii mzigo wa umwagiliaji ili ibaki na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa watu wanapata maji safi na salama mita 400 kutoka wanapoishi.


2. Idara ya Vijana tumeihamisha kutoka Wizara ya Kazi na kuihamishia Wizara ya Habari kwa sababu kuu 2.


1. Kwanza inashabihiana na michezo na utamaduni.


2. Tunataka Wizara ya Kazi ipate muda wa kutosha wa kushughulikia masuala ya ajira na wafanyakazi ambayo sasa yamepanuka.


3. Shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi zilizokuwa Wizara ya Fedha na Wizara ya Kazi zitahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.


4. Marekebisho mengine ni madogo:


1. Katika Ofisi ya Rais tunairudisha shughuli ya mahusiano na jamii hivyo tunaongeza Waziri wa Nchi ambaye pia atashughulikia shughuli zilizopanuka za Tume ya Mipango, MKURABITA na TASAF.


2. Katika Ofisi ya Waziri Mkuu tutakuwa na Waziri wa Nchi wa kushughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji wa Wananchi.


3. Katika Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya TAMISEMI tumeongeza Naibu Waziri wa kushughulikia masuala ya Elimu.


Baada ya kusema hayo nitangaze orodha yetu:


1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe


2. Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira


3.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia


4. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano): Samia Suluhu


5. . Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa


6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi


7. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu


8. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika


Naibu: Aggrey Mwanri


Naibu: Kassim Majaliwa


9. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo


Naibu: Gregory Teu


Naibu: Pereira Ame Silima


10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha


Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki


11. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani


12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe


Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi


13 . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi


14. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo


Naibu: Benedict Ole Nangoro


15. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa


Naibu: Charles Kitwanga


16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka


Naibu: Goodluck Ole Madeye


17. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige


18. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja


Naibu: Adam Kigoma Malima


19. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli


Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe


20. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu


Naibu: Athumani Mfutakamba


21. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami


Naibu: Lazaro Nyalandu


22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa


Naibu: Philipo Mulugo


23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda


Naibu: Dr. Lucy Nkya


24. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka


Naibu: Makongoro Mahanga


25. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba


Naibu: Umi Ali Mwalimu


26. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi


Naibu:Dr. Fenella Mukangara


27. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta


Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah


28. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe


Naibu: Christopher Chiza


29. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya


Naibu: Eng. Gerson Lwinge


Nitawaapisha Jumamosi tarehe 27 Novemba, 2010 saa 05:00 asubuhi






CHANZO: NIPASHE

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...