Friday, 12 November 2010

MKUU WA MKOA WA TANGA APASUA HISIA ZAKE KWA WAANDISHI



Mkuu wa mkoa wa Tanga, Said Kalembo amewataka wahariri kusaidia kupatikana kwa nyenzo za wafanyakazi wao waliopo mikoani ili kuwaondolea utegemezi.






Mkuu wa mkoa alisema utegemezi huo unawafanya wasiwe huru katika kufanyakazi zao.






Alisema yeye anaona taabu sana anapowaona waandishi wa habari wakihangaika kwa kukosa usafiri na kulazimika kuomba hapa na pale akisema kwamba hali hiyo inamuingiza mtegoni.






"Mtu hawezi kuwa huru kama anafadhiliwa kila kitu" alisistiza Mkuu huyo wa mkoa ambaye alisema pamoja na hayo ofisi yake husaidia pale inapowezekana ili waweze kuandika habari za maendeleo.






Pia katika mazungumzo yake aliwataka kuzingatia mafunzo na kutumia mafunzo hayo kuunga daraja la kuhabarisha wananchi.






"Wahariri fikirini kuwawezesha, wasaidieni wapeni nyenzo, magari na vitendea


tunawanyima uhuru kwa ajili ya fadhila, kapewa usafiri wa gari, posho na mahali pa kulala. ataandika nini" alisisitiza mkuu huyo wa mkoa.






Mkuu ambaye alikuwa akifungua warsha ya wadau katika uchaguzi uliopita alisema kwamba ipo haja ya kuangalia dhamana kama viongozi kuwajali walio chini.






Katika uchaguzi uliopita malalamiko mengi yalikuwa ni ufadhili wa vyma a kwa waandishi ambao ulionekana kuchachafya kanuni za kazi za kiuandishi.






Imeelezwa kuwa wengine waliachwa kwa sababu ya kuandika kinyume na wengine hawakujereshwa katika msafara hali inayoonesha kuna mambo gani yanaweza kutukia ukitumia usafiri na posho ya mtu unayetakiwa kumwandikia ukiwa huru.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...