Sunday, 26 December 2010

HEBU TOA MAONI!

 Je, kupeleka watoto kunyoa kwa vinyozi vinavyotumiwa na watu wazima ni salama? Nafikiri sio sahihi kungetakiwa kuwepo na vinyozi vya watoto kuliko kuwachanganya na wakubwa kama unavyojua ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngozi kama vile fangasi na mapunye kwa vile ngozi yao ni laini.

 Miradi mingi ya maji hufa muda mfupi baada ya kukamilika kutokana na kutowashirikisha wananchi, na wao kuona miradi hiyo kama si mali yao bali ni ya serikali na matokeo yake hubaki kuwa vyuma chakavu bomba ambalo halitowi maji kwa miaka mingi kutokana na ukosefu wa usimamizi madhubuti. Ingefaa pindi miradi ya maji inavyo kamilika ikabidhiwe kwa jumuiya za watumiaji maji (WUA) katika maeneo husika ili iweze kudumu. Pia ingefaa gharama za miradi wa maji (water points) ziendane na ubora wa miradi (end product) yenyewe na kuzingatia kwamba hakuna maji ya kutosha ardhini kwenye  mwamba wa maji 'watertable'.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...