Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Wasifu wa Maisha yake, akishuhudiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mwandishi wa kitabu hicho Profesa Julius Nyang'oro leo mchana Ikulu, Dar es salaam.
Nakala ya kiingereza ya Kitabu cha Wasifu wa JK kama kinavyoonekana. Picha ya chini ni Profesa Nyang'oro akitia saini nakala za kitabu hicho zilizogaiwa bure kwa wageni wote waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo. Vitabu hivyo vitaanza kuuzwa kwenye duka la vitabu la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kuanzia kesho tarehe 10-12-2010 kwa gharama ya shillingi 25,000/=
Baadhi ya wanafamilia ya Mheshimiwa Rais Kikwete wakiperuzi kurasa za kitabu cha Wasifu wa JK kilichozinduliwa leo Ikulu Dar es salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakiongea na Profesa Nyang'oro ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Wasifu wa JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Shukuru Kawambwa.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA IKULU MAWASILIANO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...
No comments:
Post a Comment