Na Friday Simbaya,
Songea
TIMU ya Soka ya Majimaji ya Songea jana ilishindwa kutamba mbele ya JKT Ruvu ya Dar es Salaam baada ya kufungwa bao 1-0 mbele ya mashabiki wake katika Ligi Kuu Soka Bara mzunguko wa pili.
Ruvu ambayo walicheza vizuri na kutumia makosa ya mabeki wa Majimaji ilipata bao lake la kuongoza katika dakika 15 ya kipindi cha kwanza.
Majimaji walipata pigo baada ya beki wa kati Mudi Mupopo kutolewa nje baada ya kupatikana na kadi za njano mbili na kufanya timu hiyo kucheza pungufu.
Timu hiyo ya Majimaji ilitokea nchini Msumbiji waliko kwenda kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali za nchini humo kwa ajili ya kujiweka tayari kwa ajili ligi kuu Bara mzunguko wa pili.
Wakitokea nchini Msumbiji ambapo walishinda baadhi ya mechi walipiga kambi kama ‘stop over’ Peramiho Songea Vijijni kabla ya kucheza na Tium ya JKT Ruvu katika Uwanja wa Majimaji Mjini Songea Mkoani Ruvuma jana.
Akizungumza na Nipashe baada ya kumalizika kwa mpira, beki wa Majimaji Evarist Maganga alisema hawakuwa na bahati licha ya kucheza nyumbani jana kutokana na kufungwa na Timu JKT Ruvu pamoja na kuwa na maandalizi ya kutosha.
Aliongeza kuwa wakazi wa Ruvuma wasife moyo kutokana na kufanya vibaya katika mechi katika Ruvu na Majimaji kwa sababu mambo mazuri yanakuja mbeleni na kuwaomba waendelee kuipa sapoti ya kutosha.
Kocha Mkuu wa timu ya Majimaji, Sebsatian Mkoma, aliwataka wakazi wa Ruvuma kuipa sapoti timu yao Majimaji ili ifufuwe matumaini ya kusonga mbele. Hata hivyo, wakazi wa Ruvuma hawakujitokeza kwa wengi kama ilivyotegemewa na timu hiyo ya wanalizombe
Nkoma ambaye amepewa majukumu ya kuliokoa jahazi hilo la Majiamaji ambalo linaonkana kuzama, alisema bado timu hiyo inanafasi ya kufanya vizuri na kubaki katika ligi kuu msimu huu.
Alisema kuwa ziara ya majimaji nchini msumbiji ilikuwa ni sehemu ya maadalizi ya kujiweka vyema kwa ajili ya ligi kuu soka bara mzunguko wa pili.
Hata hivyo, Timu ya Majimaji itamenyana na Timu ya African Lyon tarehe 20 Januari, 2011 Mjini Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment