Walimu zaidi ya 30 wa vyuo mbalimbali vya ufundi kutoka katika mikoa ya nyanda za juu (Iringa na Ruvuma) wamefanya semina ya mafunzo yaliyodumu kwa takribani wiki mbili kwa lengo la kujengewa uwezo wa namna ya kutumia mfumo mpya wa kufundishia ujulikanao kama ‘Competence Based Education and Training’ (CBET).
Akizungumza na gazeti la Mwenge, Mratibu wa vyuo vya ufundi stadi vya VETA wa nyanda za juu Bw. John Mwanja amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha walimu wa vyuo vya ufundi stadi kutumia mfumo mpya wa kufundishia yani CBET.
Mfumo huo mpya wa kufundishia (Competence Based Education and Training (CBET) unatafsiriwa kuwa ni umiliki na uendelezaji wa ustadi, ufahamu, mitazamo sahihi pamoja na uzoefu ili kujiletea mafanikio katika utendaji wa majukumu ya kimaisha.
Bw. Mwanja amesema, endapo mfumo huu mpya utatekelezwa kama ilivyokusudiwa, basi utaleta mafanikio chanya zaidi ukilinganishwa na ule mfumo uliokuwa ukitumika hapo awali kutokana na ukweli kwamba mfumo huu mpya utawawezesha wanafunzi kuendelea kutoka katika hatua moja kwenda hatua nyingine.
“Katika mafunzo ya ufundi stadi tunachukulia ustadi kama nyenzo muhimu ambayo inajumuisha elimu, uelewa, ujuzi, utendaji, mtazamo pamoja na uzoefu,” alisema Mwanja.
“Mfumo mpya wa kufundishia ni maendeleo mapya kabisa ambayo yatawapa mwanya wanafunzi wa vyuo vya ufundi kuweza kuendelea kutoka hatua moja kwenda nyingine. Hii ina maana kuwa baada ya kupata cheti cha Daraja la tatu, mwanafunzi anaweza kuendelea na ngazi ya Diploma katika chuo chochote ambacho kinatumia mfumo mpya,” aliongeza Mwanja.
Hii ni semina ya pili kufanyika katika nyanda za juu wakati semina ya kwanza ilifanyika katika wilaya ya Njombe mkoani Iringa, ambapo ilihudhuriwa na walimu wa vyuo vya ufundi wapatao hamsini na tatu 53.
Haya ni marekebisho mapya ambayo yamefanywa na VETA kwa lengo la kuboresha viwango na sifa za ufundishaji katika vyuo vya ufundi ili kukidhi ushindani uliopo katika soko la ajira.
Bw. Mwanja pia amewaasa watanzania kuwa na ustadi wa kutosha ili waweze kupambana na changamoto za ushindani uliopo katika soko la ajira.
Kila jambo lenye mafanikio halikosi pia kuwa na mapungufu, ndivyo ilivyo pia kwa huu mfumo mpya wa CBET. Mapungufu hayo yameelezwa kuwa ni uhaba wa walimu wenye viwango na sifa zinazohitajika ili kumudu mfumo mpya pamoja na ukosefu wa vitabu.
Vile vile, kwa upande wa wanafunzi wanalazimika kusoma vitabu vingi vya masomo ya ziada ambayo hayakuwepo kwenye mfumo wa awali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment